YouVersion Logo
Search Icon

BibleProject | Tafakari ya Ujio wa YesuSample

 BibleProject | Tafakari ya Ujio wa Yesu

DAY 24 OF 28

Biblia ya Kiebrania inarekodi historia ya watu wa Mungu wakipuuza tena na tena amri kuu zaidi ya kumpenda Mungu na wengine. Tunawezaje kutumaini kufanya vyema zaidi? Yesu hutusaidia anapoongeza amri mpya kuambatana na amri kuu zaidi. Amri yake mpya inaonyesha jinsi upendo wake mwenyewe wa kujitolea unavyoweza kuwawezesha wafuasi wake kuwapenda wengine.

Soma: 

Yohana 13:34, na chambua Marko 12:29-31 1 Yohana 4:9-11 

Tafakari: 

Linganisha Yohana 13:34 na Marko 12:29-31. Kuna tofauti gani kati ya amri hizi mbili? Ni kwa namna gani Mfano wa Yesu mwenyewe huhuisha na kutimiza amri kuu?

Chambua 1 Yohana 4:9-11 kwa makini. Ni maneno au vifungu vipi vya maneno vinajitokeza kwa upekee kwako? Kwa mujibu wa kifungu hiki, kwa nini Yesu alitoa maisha yake, na ni nini kinafaa kuhamasisha upendo wetu kwa wengine? 

Chukua muda kuomba kutokana na ulichojifunza leo.



Day 23Day 25

About this Plan

 BibleProject | Tafakari ya Ujio wa Yesu

BibleProject ilibuni Tafakari ya Ujio wa Yesu ili kuhamasisha watu mmoja mmoja, vikundi vidogo vidogo, na familia kusherehekea majilio, au kuwasili kwa Yesu. Mwongozo huu wa wiki nne unashirikisha video za kikatuni, mihutasari mifupi, na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia washiriki kuchunguza maana ya Biblia ya tumaini, amani, furaha, na upendo. Chagua mwongozo huu ili kujifunza jinsi maadili haya manne yamefika ulimwenguni kupitia kwa Yesu.

More