YouVersion Logo
Search Icon

BibleProject | Tafakari ya Ujio wa YesuSample

 BibleProject | Tafakari ya Ujio wa Yesu

DAY 12 OF 28

Historia ya Biblia inaonyesha jinsi wanadamu wamechagua njia zao wenyewe mbali na Mungu na kuteseka kutokana na hilo. Lakini Mungu anataka kuwa karibu na wanadamu, na anajua jinsi maumivu makali huja pale mtu anapotengansihwa na yeye, kwa hivyo alimtuma Yesu alete amani. Kupitia kwa Yesu, vitu vyote vinaweza kurejeshwa ili kuwa na umoja na Mungu tena. 

Soma:

Wakolosai 1:19-23 

Tafakari:

Kwa mujibu wa kifungu hiki, Mungu alitaka kufanya nini na alikitimiza vipi kupitia kwa Yesu? 

Fikiria mateso yote ambayo Yesu alipata na kuyashinda ili kutengeneza njia kwa wanadamu kuwa katika uwepo mtakatifu wa Mungu kwa mara nyingine tena. Acha tafakuri zako zichochee sala ili uweke wazi hisia zako za stahi na shukrani. 



Day 11Day 13

About this Plan

 BibleProject | Tafakari ya Ujio wa Yesu

BibleProject ilibuni Tafakari ya Ujio wa Yesu ili kuhamasisha watu mmoja mmoja, vikundi vidogo vidogo, na familia kusherehekea majilio, au kuwasili kwa Yesu. Mwongozo huu wa wiki nne unashirikisha video za kikatuni, mihutasari mifupi, na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia washiriki kuchunguza maana ya Biblia ya tumaini, amani, furaha, na upendo. Chagua mwongozo huu ili kujifunza jinsi maadili haya manne yamefika ulimwenguni kupitia kwa Yesu.

More