YouVersion Logo
Search Icon

BibleProject | Tafakari ya Ujio wa YesuSample

 BibleProject | Tafakari ya Ujio wa Yesu

DAY 11 OF 28

Nabii Isaya alitazamia kuwasili kwa Mwana Mfalme wa Amani, ambaye utawala wake ungeelekeza kwenye shalom ya milele. Maneno ya Isaya yalitimizwa na kuwasili kwa Yesu. Hii ndio maana ni muhimu sana ambavyo malaika walieleza kuzaliwa kwa Yesu kama “amani duniani.” 

Soma: 

Luka 2:9-15 

Tafakari:

Unafikiri ni kwa nini Mungu alitangaza kuwasili kwa Mfalme kwa wachungaji wasio maarufu? Hili linakwambia nini kuhusu tabia ya Mungu na Ufalme wake? 

Hebu jaribu kupata picha upo na wale wachungaji ule usiku. Je, ungejisikiaje? Ungejibu vipi?

Angalia maneno "juu zaidi" na "dunia" katika tangazo la kuabudu la malaika. Ni nini kilitoka juu mbinguni hadi duniani Yesu alipozaliwa? Je, hii ni habari njema kivipi? Acha tafakuri zako zichochee sala ili uweke wazi hisia zako za stahi na shukrani. 

Scripture

Day 10Day 12

About this Plan

 BibleProject | Tafakari ya Ujio wa Yesu

BibleProject ilibuni Tafakari ya Ujio wa Yesu ili kuhamasisha watu mmoja mmoja, vikundi vidogo vidogo, na familia kusherehekea majilio, au kuwasili kwa Yesu. Mwongozo huu wa wiki nne unashirikisha video za kikatuni, mihutasari mifupi, na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia washiriki kuchunguza maana ya Biblia ya tumaini, amani, furaha, na upendo. Chagua mwongozo huu ili kujifunza jinsi maadili haya manne yamefika ulimwenguni kupitia kwa Yesu.

More