BibleProject | Tafakari ya Ujio wa YesuSample
Mtume Paulo anaandika barua yake kwa Wafilipi kutoka gerezani. Anajua mateso, lakini pia anaijua amani ya Mungu. Hii ni kwa sababu amani ya Kibiblia, kama tumaini, msingi wake ni mtu na siyo hali. Paulo anatoa wito kwa wafuasi kufurahi katika Mungu wakati wote, kuomba, kutoa shukrani, na kufikiria yaliyo mazuri na kweli. Paulo anaonyesha jinsi tabia hizi zinavyoelekeza katika kupata amani ya Mungu hata katikati ya changamoto kubwa.
Soma:
Wafilipi 4:1-9
Tafakari:
Tengeneza orodha ya maagizo yote ambayo Paulo anatoa katika Wafilipi 4:1-9 (mfano “simama imara katika Bwana,” “ishi kwa upatanifu,” n.k.).
Angalia orodha yako na kisha jiulize kila mojawapo ikiwa tabia itakuwaje. Tabia hizo zitaonekana vipi kihalisia katika maisha yako ya kila siku? Unafikiri tabia hizo hatimaye zitasababishaje kupata amani ya Mungu?
Chambua mstari wa 7 na 9. Unagundua nini? Mistari hii inatuambia nini kuhusu asili ya kulinda ya amani ya Mungu? Toa shukrani zako kwa ulinzi wake sasa.
Scripture
About this Plan
BibleProject ilibuni Tafakari ya Ujio wa Yesu ili kuhamasisha watu mmoja mmoja, vikundi vidogo vidogo, na familia kusherehekea majilio, au kuwasili kwa Yesu. Mwongozo huu wa wiki nne unashirikisha video za kikatuni, mihutasari mifupi, na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia washiriki kuchunguza maana ya Biblia ya tumaini, amani, furaha, na upendo. Chagua mwongozo huu ili kujifunza jinsi maadili haya manne yamefika ulimwenguni kupitia kwa Yesu.
More