YouVersion Logo
Search Icon

Plan Info

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

DAY 2 OF 31

Cha ajabu, mtini ule wenye majani haukuwa na matunda. Haikuwa kawaida. Kwa mti kuwa na majani bila matunda hakuna faida. Yesu alikusudia kufundisha kuwa dini au watu kuishi pasipo matunda ya Roho, mwisho wake ni kifo cha milele. Hali ya Wayahudi ilifanana na pango la wanyang’anyi na mti ulio na majani pasipo matunda. Katika m.17 Yesu anasema, Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi. (ling. Isa 56:6-8, Wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu; nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote. Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao walio wake waliokusanywa). Yesu anawakumbusha kwamba ibada yenye uchaji kwenye nyumba ya sala iambatane na moyo wa kusamehe wengine kama Mungu alivyotusamehe sisi: Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu (m.25-26).

Day 1Day 3

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy