YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

DAY 4 OF 31

Yesu anaonyesha kwamba ndiye Masihi aliyetumwa na Mungu, ijapokuwa Wayahudi waliomsikia hawakutambua hilo. Shamba la mizabibu ni taifa la Israeli. Imeandikwa kwa mfano katika Isa 5:7, Shamba la mizabibu la Bwana wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! Aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! Alisikia kilio. Mwenye shamba ni Mungu. Wakulima ni mfano wa hao Wayahudi alioongea nao Yesu, na watumwa ni manabii waliotumwa na Mungu. M.9 una maonyo kwa Wayahudi waliosukumia mbali neema ya Mungu: Yule bwana wa shamba la mizabibu … atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine. M.10 waonyesha kwamba Yesu ni msingi. “Jiwe kuu la pembeni” ni mfano kuhusu Yesu. Lakini pamoja na hilo, bado watu wengi na hata wakubwa wa jamii wanamkataa. Wewe je, imani yako iko katika msingi gani?

Scripture

Day 3Day 5

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More