BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoSample
![BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F24935%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Katika karne ya kwanza, watu wengi karibu na Mediterano waliishi katika majiji yaliyojaa mno, yote yakitawaliwa na ufalme wa Kirumi. Kila jiji lilikuwa mchanganyiko mpana wa tamaduni, makabila, na dini. Kwa sababu hii, kulikuwa na mahekalu tofauti tofauti ya kutoa kafara kwa miungu tofauti tofauti, na kila mtu alikuwa na miungu tofauti ambao aliwatii. Lakini kwa kila jiji pia ungepata vikundi vya watu wachache ambao hawakuabudu miungo hao. Waisraeli, waliojulikana pia kama Wayahudi, walidai kuwa kulikuwa na Mungu mmoja wa kweli, na walitaka kumwabudu yeye pekee.
Majiji haya yote yaliunganishwa kwa safu za barabara zilizojengwa na ufalme wa Kirumi, kwa hivyo ilikuwa rahisi kusafiri ili kufanya biashara na kueneza mawazo mapya. Mtume Paulo alitumia nusu ya pili ya maisha yake akisafiri katika barabara hizi, akitangaza kuwa Mungu wa Israeli alikuwa ameteua Mfalme mpya wa mataifa, ambaye hakutawala kwa nguvu wala ushari bali kwa upendo wa kujitolea binafsi. Paulo alihudumu kama mtabiri wa habari hizi na aliwaalika watu wote kuishi chini ya utawala wa upendo wa Mfalme Yesu.
Sehemu ya tatu ya Matendo ya Mitume inahusu simulizi za ziara za Paulo na jinsi watu walivyopokea ujumbe wake. Katika sehemu hii, Luka anatuonyesha jinsi Paulo na wafanyakazi wenzake walisafiri kutoka nyumbani kwao, katika jiji la Antiokia, hadi kwa majiji yaliyoko mahali panapofaa katika ufalme. Katika kila jiji, desturi ya Paulo ilikuwa kuenda kwenye Sinagogi la Kiyahudi kwanza ili kuwaonyesha watu wake kuwa Yesu ndio utimilifu wa unabii wa Masihi wa Biblia ya Kiebrania. Baadhi waliamini ujumbe wake na kuanza kuishi chini ya utawala wa Yesu, lakini wengine walipinga ujumbe wa Paulo. Baadhi ya Wayahudi waliona wivu na kuweka mashtaka ya uongo dhidi ya wanafunzi, huku baadhi ya wasio Wayahudi wakihisi kuwa njia yao ya maisha ya Kirumi ilikuwa inatishiwa na kuwafukuza wanafunzi. Lakini upinzani kamwe haukukomesha vuguvugu la Yesu. Kusema kweli, kudhulumiwa kulisaidia kuieneza injili katika majiji mapya. Wakiwa wamejawa furaha na Roho Mtakatifu, wanafunzi waliendelea kujikaza.
Scripture
About this Plan
![BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F24935%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.
More