YouVersion Logo
Search Icon

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoSample

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

DAY 31 OF 40

Katika sehemu inayofuata ya Matendo ya Mitume, Paulo anatambua kuwa kuna baadhi ya Wakristo Wayahudi ambao wanadai kuwa Wakristo wasio Wayahudi ni lazima wawe Wayahudi (kwa kutahiriwa, kutunza Sabato, na kutimiza sheria za chakula za Kiyahudi) ili kuwa sehemu ya vuguvugu la Yesu. Lakini Paulo na Barnaba wanakataa kabisa, na wanapeleka mjadala huu kwa baraza la uongozi huko Yerusalemu ili utatuliwe. Wakiwa huko, Petro, Paulo na Yakobo (kaka yake Yesu) wanarejelea Maandishi na walichopitia ili kuonyesha kuwa mpango wa Mungu daima umekuwa kujumuisha mataifa yote. Kisha baraza linafanya uamuzi bunifu na kuweka wazi kuwa japo ni lazima Wakristo ambao si Wayahudi kuacha kushiriki katika kafara za mahekalu ya kipagani, hawahitaji kuchukua utambulisho wa kikabila wa Kiyahudi au kutii sheria za ibada na desturi za Torati. Yesu ndiye Masihi wa Kiyahudi, lakini yeye pia ndiye Mfalme aliyefufuka wa mataifa yote. Uanachama katika Ufalme wa Mungu hauna misingi ya kikabila au sheria ila tu unatakiwa kumwamini na kumtii Yesu.

Scripture

Day 30Day 32

About this Plan

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More