YouVersion Logo
Search Icon

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoSample

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

DAY 36 OF 40

Paulo anavyoendelea kuelekea Yerusalemu, anasimama njiani ili kuitembelea jamii inayokua ya wafuasi wa Yesu. Wote wanajifunza kuhusu nia yake ya kwenda katika jiji kuu na wanaipinga kwa haraka. Wanamuomba asiende, wakiwa na imani kuwa ikiwa ataenda, atafungwa gerezani au kuuawa. Lakini Paulo yuko tayari kufia anachoamini na hivyo anaendelea. Anapofika Yerusalemu, anashiriki katika tamaduni za Kiyahudi ambazo zinawasaidia wengine kuona kuwa hawapingi Wayahudi. Kwa kweli, yeye ni Myahudi mcha Mungu anayempenda Mungu wa baba zake na anaweza kutoa maisha yake kwa ajili ya Myahudi mwenzake. Lakini Wayahudi wanaona ushirika wa Paulo na watu wasio Wayahudi tu. Wanakataa ujumbe wa Paulo, wanamfukuza hekaluni, na kuanza kumpiga hadi kifo.

Warumi wanapokea habari kuwa mambo yanakuwa mabaya Yerusalemu na wanafika kwa muda na kuzuia kipigo cha Paulo. Paulo anaondolewa kutoka kwenye umati huo mkali, na anamshawishi kamanda kumpatia fursa ya kuwazungumzia watesaji wake. Akiwa bado amechubuka na kujawa damu kutokana na kipigo hicho, Paulo anasimama na kushiriki simulizi yake kwa ujasiri. Anazungumza kwa lahaja ya Kiebrania ili kuwashawishi na kujifananisha na watu wale wale waliokuwa wanataka kumuua. Wanamsikiliza hadi anapoanza kuzungumza kuhusu nia ya Mungu ya kujumuisha Mataifa (wasio Wayahudi) katika mpango wake wa wokovu. Kutokana na hili, umati unaanza kutoa matishio ya kifo kwa sauti dhidi ya Paulo mara moja. Kuna fujo, na kamanda wa Kirumi hawezi kuelewa kwa nini Wayahudi wamkasirikie Paulo sana kwa kuwaongelea Mataifa. Kwa hivyo kamanda anatambua kuwa lazima kuna mambo yaliyofichika yanayochangia hili na kuteswa zaidi kungemfanya ayaseme. Paulo anakomesha kutendewa kwake kinyume cha sheria kwa kufichua kuwa yeye ni raia wa Kirumi. Kamanda anagundua kuwa anaweza kuwa mashakani kwa kumuumiza Mrumi, hivyo Paulo anaachiliwa upesi kutoka rumande na kusindikizwa hadi kwenye mkutano wa kusikiliza kesi mahakamani ambapo anaweza kujitetea mbele ya viongozi wa dini waliomshutumu.

Day 35Day 37

About this Plan

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More