BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoSample
Baada ya Paulo kukata rufaa ili ashtakiwe huko Rumi, Festo anamweleza Mfalme Agripa yote yaliyofanyika. Hili linamvutia Mfalme na anaamua kuwa anataka kusikia kutoka kwa Paulo yeye mwenyewe. Kwa hivyo siku inayofuata, Luka anatuambia kuwa kila kitu kinapangwa na watawala wengi muhimu wanaandamana na Agripa ili kumsikia Paulo akitoa ushahidi. Kisha Luka anaandika maelezo ya tatu kuhusu simulizi ya Paulo na utetezi wake. Lakini wakati huu, rekodi ya Luka inaonyesha Paulo akitoa maelezo ya ndani zaidi ya kilichofanyika siku aliyokutana na Yesu aliyefufuka. Wakati mwanga unaopofusha ulipong'aa kandokando ya Paulo na akasikia sauti kutoka Mbinguni, ilikuwa ni Yesu akizungumza kwa lahaja ya Kiebrania. Yesu alimuita ili ashiriki uzoefu wake wa kubadilisha na Mataifa na Wayahudi, ili wao pia waone mwanga wa msamaha wa Mungu na kutoroka uovu wa Shetani. Paulo alitii amri ya Yesu na kuhubiri ukweli kuhusu mateso na kufufuka kwa Yesu na mtu yeyote ambaye angesikiliza, akiwaonyesha kutoka katika Maandiko ya Kiebrania kuwa kwa kweli Yesu alikuwa Masihi aliyesubiriwa kwa muda mrefu, Mfalme wa Wayahudi. Festo hawezi kuamini simulizi ya Paulo, na anapiga kelele kuwa Paulo ana kichaa. Lakini Agripa anaona uwiano kwa maneno ya Paulo na anakiri kuwa anakaribia kuwa Mkristo. Japo Festo na Agripa hawakubaliani kuhusu hali ya kiakili ya Paulo, wote wanakubali kuwa Paulo hakufanya chochote kinachostahiki kifo au kufungwa gerezani.
Scripture
About this Plan
Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.
More