YouVersion Logo
Search Icon

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoSample

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

DAY 33 OF 40

Wayahudi wengi walikuwa na matarajio maalumu juu ya Masihi wao. Walifikiri Mfalme wao aliyeahidiwa angechukua kiti cha enzi na kuwaokoa kutoka katika ukandamizaji wa Kirumi. Hivyo Yesu alipokuja na kuanza kushirikiana na waliotengwa katika jamii na kutangaza Ufalme wa Mungu kwa unyenyekevu, baadhi hawakumtambua kama Masihi na hata kupinga utawala wake vikali. Kwa kinaya, upinzani wao ulikuwa zana ambayo Mungu aliitumia ili kuasisi utawala wa Yesu, na kupitia kusulubishwa, kufufuka, na kupaa mbinguni kwake, Yesu alitawazwa mbinguni kama Mfalme wa Wayahudi na mataifa yote. Katika sehemu inayofuata, Luka anatuambia kile ambacho Paulo alipitia akihubiri ujumbe huu huko Thesalonike, Berea, na Athene.

Akiwa Thesalonike, Paulo alithibitisha kutoka katika Maandiko ya Kiebrania kuwa manabii walisema daima kuwa ni lazima Masiha ateseke na afufuke ili atawale kama Mfalme. Paulo alionyesha kuwa Yesu alilingana na unabii ulionenwa na manabii wa kale, na wengi walishawishika. Jinsi hadhira ya Paulo ilivyokua, baadhi ya Wayahudi wenye wivu waliwachochea washawishi wa jiji wamshutumu Paulo kuwa amebadilisha ulimwengu mzima juu chini kwa kutangaza Mfalme mpya. Makoloni ya Kirumi hayakutaka kumfadhaisha mfalme, kwa hivyo hii ilikuwa shutuma kali ambayo ingemfanya Paulo auawe. Paulo alitumwa kutoka Thesalonike ili ahubiri habari njema kuhusu Ufalme wa Yesu katika jiji la Berea badala yake. Akiwa huko, Paulo alipata wanaume na wanawake waliokuwa na hamu ya kusikiliza, kusoma, na kuhakikisha kuwa ujumbe wake ulikuwa unalingana na Maandiko ya Kiebrania. Wengi ndani ya Berea walianza kumfuata Yesu, lakini safari ya Paulo ilifupishwa wakati wanaume wa Kiyahudi kutoka Thesalonike walisafiri hadi Berea ili kumfukuza kutoka huko pia. Hili lilimfanya Paulo aende Athene, ambako aliingia katikati ya soko la mawazo ili kueleza utambulisho wa kweli wa “mungu wao asiyejulikana" na maana ya kufufuka kwa Yesu.

Scripture

Day 32Day 34

About this Plan

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More