BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoSample
Katika sehemu hii ya Matendo ya Mitume, ripoti mpya zinawasili kuhusu idadi ya watu wasio Wayahudi wanavyomfuata Yesu katika jiji la biashara la Antiokia. Hivyo wanafunzi walio Yerusalemu wanamtuma mfuasi wa Yesu anayeitwa Barnaba kuangalia kinachofanyika. Anapofika Antiokia, anakuta watu wengi kutoka kote duniani wamejifunza habari za Yesu. Kuna wafuasi wengi wapya na kazi kubwa ya kufanya, hivyo Barnaba anampatia Sauli nafasi ya kuja kufundisha naye Antiokia kwa mwaka mmoja.
Antiokia ndiyo sehemu ambapo wafuasi wa Yesu wanaitwa Wakristo kwa mara ya kwanza, kumaanisha “wa Kristo.” Kanisa la Antiokia ndio jamii ya kimataifa ya Yesu ya kwanza. Sehemu kubwa ya Kanisa haijumuishi Wayahudi wa kimasihi kutoka Yerusalemu tena; sasa ni vuguvugu la makabila mengi linaloenea kwa kasi kote duniani. Rangi za ngozi zao, lugha, na tamaduni ni tofauti, lakini imani yao ni sawa, ikiwa na msingi kwa habari njema za Mfalme wa mataifa yote, Yesu aliyesulubishwa na kufufuka. Lakini ujumbe wa Kanisa na njia yao mpya ya maisha inachanganya, na hata kutishia, kwa raia wa kawaida wa Roma. Na Mfalme Herode, mfalme kibaraka wa ufalme wa Kirumi, anaanza kuwadhulumu na kuwaua Wakristo. Mfalme anavyozidi kuona kuwa kuwatesa Wakristo kunawafurahisha baadhi ya viongozi wa Kiyahudi, ndivyo anavyoendelea kufanya hivyo, jambo ambalo hatimaye linasababisha kukamatwa kwa Petro. Maisha ya Petro yako hatarini, lakini marafiki zake wanaombea kuachiliwa kwake kwa bidii. Usiku kabla ya siku ambayo Herode alikuwa amepanga kumtoa Petro kwa umati mkali, malaika anatembelea chumba chake gerezani, anavunja minyororo yake na kumwondoa gerezani.
Scripture
About this Plan
Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.
More