YouVersion Logo
Search Icon

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoSample

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

DAY 26 OF 40

Katika sehemu hii inayofuata, Luka anaonyesha kuwa kuuliwa kwa huzuni kwa Stefano hakuwezi kusimamisha vuguvugu la Yesu. Kwa kweli, kuteswa huku kunasababisha kutawanyika kwa wanafunzi nje ya Yerusalemu hadi kwa maeneo yasiyo ya Kiyahudu yaliyo karibu na Uyahudi na Samaria. Wanafunzi wanavyoenda nje, wanaleta ujumbe wa Ufalme wa Mungu, kama tu Yesu alivyowaamuru kufanya. Wanafunzi wanatangaza habari njema ya Yesu, na watu wanaachiliwa huru na kuponywa kimiujiza. Mchawi maarufu anaona kuwa uwezo wa Mungu ni mkuu zaidi ya wa kwake, na afisa wa makao ya malkia wa Uhabeshi anabatizwa. Ufalme unaenea na hakuna kinachoweza kuangusha mpango wa Mungu, sio hata mwanaume anayeitwa Sauli, kiongozi wa dini anayewazoa wafuasi wa Yesu kutoka majumbani kwao na kuwafunga gerezani.

Sauli anaposafiri kwenda Dameski akiwatafuta wanafunzi ili awafunge, anasimamishwa na mwanga unaompofusha na anasikia sauti kutoka mbinguni. Ni Yesu aliyefufuka mwenyewe anamuuliza Sauli ni kwa nini anapigana naye. Kukutana huku na ishara za kushangaza zinazofuata kunabadilisha msimamo wa Sauli kabisa kuhusu utambulisho wa Yesu. Mipango ya Sauli inabadilishwa kikamilifu. Badala ya kuwatesa wafuasi wa Yesu huko Demeski, Sauli anakuwa mmoja wao na anaanza kumtangaza Yesu kama Mwana wa Mungu mara moja.

Day 25Day 27

About this Plan

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More