Soma Biblia Kila Siku 12/2020Sample
Tumaini la Kikristo, kwamba Yesu aja upesi, halitufundishi ulegevu na uzembe ambao tokeo lake ni njaa na kuwasumbua wengine (m.11, Waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine), bali hutufanya tutende kazi kwa utulivu (m.12, Watende kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe) ili tujipatie chakula na hata uwezo wa kutenda mema (m.13, Msikate tamaa katika kutenda mema). Paulo alishuhudia hiyo kwa mfano wake mwenyewe, akikaa kwao (m.7-9, Hatukuenda bila utaratibu kwenu;wala hatukula chakula kwa mtu ye yote bure; bali kwa taabu na masumbufu, usiku na mchana tulitenda kazi, ili tusimlemee mtu wa kwenu awaye yote.Si kwamba hatuna amri, lakini makusudi tufanye nafsi zetu kuwa kielelezo kwenu, mtufuate). Wale wasiotaka kufanya kazi, wasipatiwe chakula, bali waonywe (m.10 na 12, ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula. … watende kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe). Wasipojirekebisha, waumini wasijenge urafiki nao (ni maana ya msizungumze naye; m.14), bali wazidi kuonywa ili waone aibu, yaani kutubu (m.14-15, Apate kutahayari; …msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu).
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More