Soma Biblia Kila Siku 12/2020Sample
Wathesalonike wanahimizwa wadumu katika maombi. Maombi yetu hayabadilishi mapenzi ya Mungu wala hayamlazimishi, bali yatufungua sisi, neno la Bwana liendelee kuingia kwetu na hata kwa wale tuwaombeao (m.1, tuombeeni, neno la Bwana liendelee). Neno la Mungu linatukuzwa, linapobadilisha maisha ya watu walipokeao. Paulo akiongeza vile vile kama ilivyo kwenu (m.1), anasema kwamba Wathesalonike wenyewe ni mfano wa hiyo (taz. 1 The 1:7-10, Mkawa kielelezo kwa watu wote waaminio katika Makedonia, na katika Akaya.Maana kutoka kwenu neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea; hata hatuna haja sisi kunena lo lote.Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaziacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai, wa kweli;na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni Yesu, mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja). Kwa njia hiyo Mungu hutulinda na waovu (m.2-3, Tukaokolewe na watu wasio haki, wabaya; maana si wote walio na imani.Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu) na kujaza mioyo yetu na upendo na uvumilivu (m.5, Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na saburi ya Kristo).
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More