YouVersion Logo
Search Icon

Plan Info

Soma Biblia Kila Siku 12/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 12/2020

DAY 2 OF 31

Kwanza binadamu hakuruhusiwa kula wanyama (Mwa 1:29, Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu). Ila sasa Mungu humruhusu, isipokuwa damu yake: Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote (m.3; ling. 1 Tim 4:4-5, Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba). - Bali mtuni tofauti kabisa na wanyama! Kumwua mwanadamu ni kitu kibaya mno machoni pa Mungu:Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu; maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu(m.6)!

Scripture

Day 1Day 3

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 12/2020

Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mun...

More

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy