YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 10/2020

DAY 18 OF 31

Siku ya sitaMungu akaumba wanyama, vitu vitambaavyo na mtu. Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana (m.31). Uumbaji wa Mungu haukuwa na kasoro lolote! Kifo k.m. hakikuwepo, maana wanadamu na wanyama hawakupangiwa kula nyama,yaani, kuuana. Bali wanadamu, wanyama na kila kitu kitambaacho walipewa matunda, mimea na majani kwa ajili ya kula (m.29-30). Na Mungu atakapoumba mbingu na dunia kwa upya, hali itarudia tena kuwa ile aliyokusudia Mungu awali! Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.Ng'ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng'ombe.Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira.Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji yanavyoifunika bahari(Isa 11:6-9).

Day 17Day 19

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 10/2020

Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More