YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 13

13
Sala ya ukombozi kutoka kwa adui
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 # Kum 31:17; Ayu 13:24; Zab 22:1; Isa 59:2 Ee BWANA, utanisahau hadi lini, hata milele?
Hadi lini utanificha uso wako?
2Nitakuwa na wasiwasi rohoni mwangu hadi lini,
Nikihuzunika moyoni mchana kutwa?
Adui yangu atatukuka juu yangu hadi lini?
3 # Ezr 9:8; Zab 18:28; Lk 2:32; Ufu 21:23; Zab 76:5,6; Isa 37:36; Yer 51:39; Efe 5:14 Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie;
Uyatie nuru macho yangu,
Nisije nikalala usingizi wa mauti.
4Adui yangu asije akasema, Nimemshinda;
Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa.
5 # 2 Nya 20:12 Lakini mimi nimezitumainia fadhili zako;
Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.
6Naam, nitamwimbia BWANA,
Kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu.

Currently Selected:

Zaburi 13: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in