YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 12

12
Ombi la msaada wakati wa dhiki
Kwa mwimbishaji: kwa kufuata Sheminithi. Zaburi ya Daudi.
1 # Isa 57:1 Tuokoe, ee BWANA, maana hamna tena amchaye Mungu
Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu.
2Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe,
Wenye midomo ya kujipendekeza;
Husemezana kwa mioyo ya unafiki;
3BWANA ataikata midomo yote ya kujipendekeza,
Na ulimi unenao maneno ya kiburi;
4Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda;
Midomo yetu ni yetu wenyewe,
Ni nani aliye bwana juu yetu?
5 # Kut 3:7,8 Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge,
Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji,
Sasa nitasimama, asema BWANA,
Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
6 # 2 Sam 22:31; Zab 18:30; Mit 30:5 Maneno ya BWANA ni maneno safi,
Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi;
Iliyosafishwa mara saba.
7Wewe, BWANA, ndiwe utakayetuhifadhi,
Utatulinda na kizazi hiki milele.
8Wasio haki hutembea pande zote,
Huku ufisadi ukitukuka kati ya wanadamu.

Currently Selected:

Zaburi 12: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in