KutakaMfano
Mungu unayezidi kumwamini kuwa na, katika mwanga wake, kuamini mwenyewe kuwa siyo muhimu kwa uhusiano wa karibu, ni muhimu kwa ushindi. Soma tena KumbuKumbu la Torati 33:29 na utaona vifungo vya ushindi na utambulisho vimefungwa pamoja. Ni kwa sababu tuu ya ngao na upanga wa Mungu wao wanaweza kusimamia dhidi ya adui zao.
Mfanano wa waamini wa Agano Jipya katika Waefeso 6:10-17 ni mzuri sana.
Wafunge pamoja:
Kila kushhindwa kwa mwana wa Mungu katika vita kunaweza kuhesabiwa kwa sababu moja au mbili:
1) Kile ambacho hatujajifunza au 2) jinsi gani tumedanganywa. Ushindi wetu na kushindwa kwetu kunasukumwa na imani yetu. Na ndivyo kilivyo kina cha uhusiano wetu wa karibu na Mungu.
Kila mara tunapochagua dhambi, tunatenda katika uongo ambao mara nyingi unakuwa hivi: Ulimwengu ni mtoaji na Mungu anachukua. Biblia ni kielelezo cha Mungu wa kweli, kuhusu sisi wenyewe, mambo yetu yaliyopita, kuhusu wengine, kuhusu maadui zetu, kuhusu ulimwengu huu na ule ujao. Kutembea katika kweli kama mwana wa Mungu na kuweza kutambua uongo uliojificha kwenye mwanga wa nyoka, anza kujiuliza juu ya imani yako kwa kipimo hiki: Ni nani alikuambia? wachungaji, na waalimu ni zawadi kwetu, na tunatakiwa kustawi chini ya mafundisho yao. Hata hivyo, inategemea kama wanayofundisha yanaendana na kile Mungu anachosema.
Ni wazi hatujifunzi utambulisho wetu kutoka kwa wachungaji na walimu peke yao.
Utambulisho wetu unafanywa na wazazi wetu, ndugu zetu, wenzetu, walimu, vyombo vya usalama, shule, uzoefu wetu, mazingira, na hofu. Mfano wa mahojiano kuelezea nachokisema:
Niambie mambo machache kuhusu wewe.Naam, mimi ni mpumbavu. Sina bahati. Mzembe. Si mtunzaji wa fedha. Sipendezi. Sipendwi. Sina akili hata kidogo. Mimi ni wa kushindwa tu.
Ni nani alikuwa hivyo? Mama yangu.
Au alikuwa mpenzi wako za zamani? Wanafunzi wenzako darasani? Ugonjwa wako? Ulijiambia mwenyewe?
Sema ukweli na mifupa yako yenye afya, kila " Ni nani alikuambia?" inahitaji kuifuatilia kwa Mungu katika maandiko, na, kama hailingani, unahitaji kuitupilia mbali. Adamu na Hawa waliangukia katika uongo na kuurudisha ubinadamu katika udongo. Kushindwa kwako kulikuwa kwa haraka na kukubwa na yote hayo kwa sababu ya utambulisho bandia. Udanganyifu ni mwizi siku zote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Katika siku hizi 7 za kusoma na kujifunza, Beth Moore anatumia maswali kutoka katika Maandiko Matakatifu ili kukuongoza kwenye uhusiano wa ndani zaidi na Yeye anayekujua vizuri. Alama za uandishi zilizopotoka mwisho wa sentensi zinaonyesha udadisi, hamu au labda wasiwasi. Swali ni mwaliko toka katika hali hatarishi hadi ukaribu wa ndani zaidi. Biblia haiachi ukaribisho huo. Mara kwa mara tunaona watu wa Mungu wakimuuliza Muumbaji wao maswali. Na pia tunamwona Mungu Muumbaji akiuliza maswali kwa viumbe wake. Changamoto ni kupokea mwaliko. Jifunze kuchimba ndani ya Neno la Mungu, kujibu maswali ya Mungu, na kuleta maswali mbele Zake. Ruhusu alama za uandishi zilizopotoka ziwe ramani ya kusogeza uhusiano wako na Baba yako kuwa wa ukaribu zaidi.
More