Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

KutakaMfano

The Quest

SIKU 2 YA 7

Mungu tayari anajua moyo wako. Amekwisha soma mawazo yako. Na utakapokuwa umemaliza masomo yako, unaweza kuchana vijarida vyako au kuchoma, lakini kuanzia sasa na baadaye, utakuwa ni wewe halisi na Bwana wa mbingu. Kuna kitu zaidi unakitafuta kuliko majibu. Unataka ufunuo. Uliumbwa kwa ajili ya huo. Na mimi vivyo hivyo.

Iweje Mungu amuulize mtu maswali wakati tayari anayajua majibu? Yawezekana siku moja atatoa maelezo mengi, lakini mara kwa mara maandiko yanatuambia hiki: Mungu, muumbaji wetu, Mkombozi, na Mfalme, anataka mahusiano na uumbaji wake pamoja na shida zetu zote na mashaka na kushindwa kwetu. Na siyo tuu mahusiano. Anataka ushirikiano. Anataka urafiki.

Na wewe. Si kwa vile ulivyotaka kuwa au kufanya kama uko mbele ya watazamaji. Wewe.

Soma Mwanzo 1:26–2:17 na 3:1-9, kumbuka—weka alama—kila mstari wenye maneno Mungu alisema moja kwa moja na Adamu. Mungu alimuuliza swali gani katika Mwanzo 3:9?

Sasa, chukua nafasi ya Adamu na upate maswali ya kimungu. Uko wapi? Una sehemu ya kwenda, lakini njia sahihi uendako inaanza mahali ulipo. Katika kijarida, mwandikie Mungu moja kwa moja ukimwelezea mahali ulipo katika maisha sasa. Kama uko mahali ambapo ni pazuri kiasi, mweleze juu ya mahali hapo. Lakini mweleze kama mtu ambaye anakujali na angefurahi pamoja na wewe. Kwa upande mwingine unaweza kuwa uko sehemu ambayo imekuchosha, au muhimu, ya kuumiza, au ya upweke.

Elezea mahali ulipo kwa uhuru wa kujieleza kwa Mungu. Yawezekana, uko sehemu nzuri zaidi kuliko sehemu jirani na wewe. Mweleze magumu yote.

Ukweli usemwe, yawezekana unatamani ungemuuliza Mungu swali hilo hilo: "Bwana, uko wapi? Ulikuwa wapi siku za karibuni?" au " ulikuwa wapi wakati...?" Yawezekana unajua majibu kibiblia au kitheolojia. Unakumbuka ahadi zilizoko kwenye maandiko kwamba hata kuacha wala kukupungukia, lakini moyo wako unahisi kama hapatikani. Kwa kweli unaweza kumuuliza yuko wapi au, kama inahusu wakati uliopita, alikuwa wapi.

Malizia kuandika kijarida chako leo na Zaburi 139:7-10, kwa kuiga maneno kama yalivyo ya mtunga zaburi au kuandika kwa maelezo yake kwa maneno yako mwenyewe.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

The Quest

Katika siku hizi 7 za kusoma na kujifunza, Beth Moore anatumia maswali kutoka katika Maandiko Matakatifu ili kukuongoza kwenye uhusiano wa ndani zaidi na Yeye anayekujua vizuri. Alama za uandishi zilizopotoka mwisho wa sentensi zinaonyesha udadisi, hamu au labda wasiwasi. Swali ni mwaliko toka katika hali hatarishi hadi ukaribu wa ndani zaidi. Biblia haiachi ukaribisho huo. Mara kwa mara tunaona watu wa Mungu wakimuuliza Muumbaji wao maswali. Na pia tunamwona Mungu Muumbaji akiuliza maswali kwa viumbe wake. Changamoto ni kupokea mwaliko. Jifunze kuchimba ndani ya Neno la Mungu, kujibu maswali ya Mungu, na kuleta maswali mbele Zake. Ruhusu alama za uandishi zilizopotoka ziwe ramani ya kusogeza uhusiano wako na Baba yako kuwa wa ukaribu zaidi.

More

Tungependa kumshukuru Beth Moore na LifeWay Women kwa kutupa mpango huu. Kwa taarifa zaidi tembelea: http://www.lifeway.com/thequest