KutakaMfano
Tumeangalia maswali mawili kati ya matano yaliyokarabatiwa:1) Uko wapi? na 2) Ni nani aliyekuambia hivyo? Swali letu la tatu ni lile ambalo Yesu aliuliza katika Yohana 1:38: “Mnatafuta nini?” Hapendezwi na majibu yetu kwa majibu ambayo tunadhani anataka kusikia. Yesu anaweza kukabiliana na ukweli wetu. Anajua majibu sahihi kwa swali, "Mnatafuta nini?" ni "shida". au fedha. au usalama. au ngono. au mali. Wakati mwingine ushuhuda mkubwa unaweza kuwa, "Nilikuwa natafuta----------------na nimempata Yesu."
Mwanamke msamaria katika Yohana 4 hajuka kisimani akimtafuta Yesu. Alikuja kutafuta maji, na akamtambulisha kwenye maji yaliyo hai. Hakukataliwa kwa kutafuta kitu kisicho sahihi. Yesu alitumia kitu alichokuwa anakitafuta ili kumleta katika hitaji la ndani la moyo wake: Mwokozi atakayezima shida, kusamehe dhambi zake, na kumpa heshima. Masihi aliyejua taarifa sahihi za habari zake na hakuwa tayari kukubali upotoshaji wake.
Vivyo hivyo, Yesu alikuwa kitu cha mwisho ambacho Sauli alifikiria anakitafuta wakati alipomkimbilia katika bara bara iendayo Dameski. Alikuwa hamuwindi Yesu. Likuwa akiwawinda wafuasi wa Yesu. Unaona, waombao hupokea hata kama wanapokea tofauti na walivyoomba. Watafutao huona hata kama wanachokiona kinatofautiana na walichokuwa wanakitafuta. Mlango hufunguliwa kwa abishaye hata kama mwenyeji asiyetarajiwa atafungua kitasa cha mlango. Huona chini ya mahitaji yetu ya muda mfupi nahuona kitu ambacho tunakihitaji zaidi tunapokaribia ule mstari wa mwisho. Isaya 46:10 inashika dhana kubwa inayolingana na hitaji letu: Mungu anajua mwisho toka mwanzoni. Maneno hayo matano ndiyo hubadili mchezo katika mashindano haya ya Olimpiki. Yanaweka imani katika kifua cha mhitaji.
Ni shauku gani inayochochea ndani yako? Nini matamanio yako? Ni yepi katika hayo yameendelea bila kutoshelezwa? Mwandikie Mungu na umwambie kile unachotamani. Unachohitaji. Mwambie matamanio yanayokusukuma. Unaweza kujikuta kwamba Mungu alikwisha kuyapanda baadhi ya matamanio hayo moyoni mwako kwa mkono wake mwenyewe.
Soma maneno ya Zaburi 38:9 kwa sauti kwa Yesu unapomalizia. Yatafakari. Yakariri. Acha kweli hii iwe ni hema unayoweza kupumzikia unapoendelea na safari yako.
Kuhusu Mpango huu
Katika siku hizi 7 za kusoma na kujifunza, Beth Moore anatumia maswali kutoka katika Maandiko Matakatifu ili kukuongoza kwenye uhusiano wa ndani zaidi na Yeye anayekujua vizuri. Alama za uandishi zilizopotoka mwisho wa sentensi zinaonyesha udadisi, hamu au labda wasiwasi. Swali ni mwaliko toka katika hali hatarishi hadi ukaribu wa ndani zaidi. Biblia haiachi ukaribisho huo. Mara kwa mara tunaona watu wa Mungu wakimuuliza Muumbaji wao maswali. Na pia tunamwona Mungu Muumbaji akiuliza maswali kwa viumbe wake. Changamoto ni kupokea mwaliko. Jifunze kuchimba ndani ya Neno la Mungu, kujibu maswali ya Mungu, na kuleta maswali mbele Zake. Ruhusu alama za uandishi zilizopotoka ziwe ramani ya kusogeza uhusiano wako na Baba yako kuwa wa ukaribu zaidi.
More