Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wimbo: Neema katika Hadithi YakoMfano

Wimbo: Neema katika Hadithi Yako

SIKU 2 YA 5

Niliwahi Kupotea

Hadithi ya Newton imefupishwa na mstari huu mmoja, nilipotea zamani, lakini sasa nimepatikana.

Tunaweza kupatikana tu ikiwa tunajua tumepotea; tunapogundua kuwa kuna njia sahihi, lakini hatuko juu yake. Hapo ndipo tunapofahamu hitaji letu la kupatikana.

Ukweli ni kwamba, bila Yesu, sote tumepotea. Tumepotea kiroho, ingawa hatujapotea kimwili.

Biblia inaeleza maana ya kupotea:

“Kwa habari zenu, mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu, 2 ambazo mlizitenda mlipofuatisha namna ya ulimwengu huu na za yule mtawala wa ufalme wa anga, yule roho atendaye kazi sasa ndani ya wale wasiotii.” (Waefeso 2:1-2).

Tunapopotea, tunaishi katika dhambi—mambo mabaya tunayofanya yanayopingana na sheria kamilifu ya Mungu. Hatujui tofauti kati ya dhambi na haki. Hatumfuati Yesu, bali “njia za ulimwengu huu” badala yake. Njia ya ulimwengu uhaidi uzima, lakini inaongoza tu kwenye uharibifu, na, hatimaye, kifo.

Hakuna mtu aliyepotea anayeweza kuwa nyumbani kwa wakati mmoja. Tunapopotea kiroho, hatuishi nyumbani na Yesu. Yesu anaahidi kwamba Baba na Yeye mwenyewe hufanya makao yao pamoja na wale wanaowapenda (Yohana 14:23).

Habari njema ni kwamba kuna njia ya kupatikana. Hatuhitaji kuishi nje ya nyumba ya Mungu milele. Hakuna kufuli kwenye mlango. Lakini, tunaweza kupatikana tu ikiwa mtu mwingine atakuja na kutupata.

Ndiyo maana Yesu alikuja. Katika Luka 19:10 anasema, “Kwa maana Mwana wa Adamu amekuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.”

Yesu anawatafuta na kuwaokoa wale waliopotea, akiongoza kila mtu nyumbani kwake. Ili kwamba pamoja na John Newton, tunaweza kuimba, nilipotea zamani, lakini sasa nimepatikana.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Wimbo: Neema katika Hadithi Yako

Labda umesikia neno "neema", lakini linamaanisha nini haswa? Neema ya Mungu inawezaje kuokoa na kubadilisha maisha yetu? Jifunze jinsi neema hii ya ajabu hukutana nasi mahali tulipo na kubadilisha hadithi zetu.

More

Tungependa kumshukuru Pulse Evangelism kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://pulse.org