Wimbo: Neema katika Hadithi YakoMfano
Neema katika kudondoka kwetu
Neema ni kwa kila mtu. Ikiwa unafuata sheria zote, au makosa yako yamekuweka gerezani. Iwe wewe ni mraibu wa ununuzi, au uraibu wa dawa za kulevya. Ikiwa familia yako inakupenda, au kila mtu katika maisha yako amekuacha.
Iwe unafikiri unastahili, au unafikiri umedondoka mara nyingi sana—neema ni kwa ajili yako.
Neema si kwa ajili ya ukamilifu wako, wewe uliyejiweka sawa, na uliye msafi. Neema ni ya niliyeshindwa tena, hakuna mtu angeweza kunipenda, nimeenda mbali sana, wewe.
Yohana 8 inasimulia kisa cha mwanamke aliyekamatwa katika tendo la uzinzi. Viongozi wa kidini wa wakati huo walipata mwanamke ambaye alikuwa amelala na mwanaume ambaye hakuwa mume wake. Sheria ilitaka kwamba adhabu ya uzinzi ni kifo.
Yesu alikuwa akifundisha katika sehemu za hekalu wakati viongozi walipomleta mwanamke huyu mbele Yake. Tunaweza kuwazia aibu na woga alioona mwanamke huyo alipotupwa chini mbele ya Yesu. Shutuma zikivuma masikioni mwake. Hukumu inayomzunguka. Alijua alichokuwa amefanya. Alijua amechanganyikiwa.
Umati uliposhika mawe mikononi mwao, maneno yaliyotoka kinywani mwa Yesu yalishtua: “Kama kuna mtu yeyote miongoni mwenu ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe.” (Yohana 8:7). Na kila mmoja akaangusha mawe yake mmoja baada ya mwingine mpaka Yesu pekee na yule mwanamke wakabaki.
Hakumfokea, hakumdhihaki, wala hakumhukumu. Badala yake, Yesu aliingia katika hali ya kuvunjika kwake, na kumwambia kwamba hakumhukumu, na akamwalika kuishi maisha tofauti (Yohana 8:10-11).
Yesu alimpa mwanamke huyu kitu ambacho alihitaji zaidi, lakini hakutarajia - neema. Hakuogopa kuingia kwenye kuanguka kwake. Hakumfanya aende kujisafisha kabla hajazungumza naye. Alikuja kwake jinsi alivyokuwa na kumpa neema ambayo sio tu iliokoa maisha yake, lakini iliyabadilisha.
Neema haiogopi kudondoka. Yesu anatualika tuje kwake na dhambi zetu zozote kwa sababu neema yake hutusafisha na kutuongoza nyumbani.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Labda umesikia neno "neema", lakini linamaanisha nini haswa? Neema ya Mungu inawezaje kuokoa na kubadilisha maisha yetu? Jifunze jinsi neema hii ya ajabu hukutana nasi mahali tulipo na kubadilisha hadithi zetu.
More
Tungependa kumshukuru Pulse Evangelism kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://pulse.org