Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yesu Ni Nani?Mfano

Yesu Ni Nani?

SIKU 2 YA 5

Yeye ndiye Muumba.

‘Vyote vilifanyika kwa huyo,wala pasipo huyo hakikufanyika cho chote kilichofanyika.’(Yohana 1:3).

Moja ya kumbukumbu zangu za Krismasi ni wakati nilisimama na mama yangu, tukiangalia mapambo ya Krismasi katika dirisha kubwa. Maonyesho hayo ya ajabu yalitengenezwa kutokana na vifaa vilivyopatikana wakati huo: ubao, karatasi ya gundi, gundi, na taa kidogo. Bali kila dirisha liliwakilisha kitabu cha hadithi ya furaha ya majira.

Mapambo ya leo yanashangaza na ni yenye mchanganyiko wa ubunifu wa muziki, taa, na roboti. Waundaji wa uwakilishi wa kipekee wa karne ya 21 wana karama ya ubunifu na uwezo wa kuendesha miundo iliyowekwa inayofafanua.

Hata hivyo, hakuna uumbaji wa mwanadamu unaoweza kuanza kugusa uumbaji wa Mungu. Katika Injili ya Yohana, tunakutana na ufunuo mzito: Yesu sio tu ni Mwokozi wa ulimwengu, bali vile vile ni Muumba wa vitu vyote.

Ujumbe wa Krismasi ni Muumba anafanyika aliyeumbwa. Muumba aliingia katika uumbaji wake, akiivaa hali ya mwanadamu, jambo la ajabu kuu.

Krismasi hii, tunakiri Zawadi ya kweli ya Krismasi – kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

Majira haya, tunaweza kufurahia maonyesho na mapambo ya kipekee ya Krismasi, hebu tukumbuke na tutafakari kuhusu yeye ambaye aliumba nyota na akaleta uzima, uzima tele duniani hapa, Yesu. Yesu muumba, anatualika tumtizame Yeye, sio kama onyesho katika dirisha dukani linalokamata fikra zetu, bali kama Mkombozi na Rafiki.

Nazingatia nini majira ya Krismasi hii na hii inaonyesha namna gani imani yenye ujasiri?

-

Mungu Baba, nakutukuza kwa uaminifu wako toka kizazi hadi kizazi. Neema, nguvu na upendo wako vyaonekana wazi katika majira haya kupitia kwa mwana wako, Yesu Kristo. Yaweke macho yangu yamzingatie Yesu – onyesho kuu sana la upendo, aliyeingia kwa unyenyekevu katika uumbaji wake ili atukomboe.

Amina.

Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Yesu Ni Nani?

Tunapoingia Ujio, tukisubiri na kujiandaa kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu, tukiiandaa mioyo yetu kwa ajili ya Krismasi, maneno ya Mtakatifu Yohana yanatutangazia hali ya uungu na uwepo wa milele wa Yesu, aliyekuja ‘kusimamisha hema lake’ kati yetu.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org