Yesu Ni Nani?Mfano
Yeye ndiye Neno.
‘Hapo mwanzo kulikuwapo Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.’ (Yohana 1:1-2).
Tunapoingia Ujio, tukisubiri na kujiandaa kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu, tukiiandaa mioyo yetu kwa ajili ya Krismasi, maneno ya Mtakatifu Yohana 1:1-2 yanatutangazia hali ya uungu na uwepo wa milele wa Yesu, aliyekuja ‘kusimamisha hema lake’ kati yetu.
Wayahudi walikuwa wanasubiri Masihi aje. Na hatimaye alipokuja, vile vile kama alivyotabiri, hawakumtambua Yesu kama Masihi: ‘Alikuja kwake wala walio wake hawakumpokea.’(Yohana 1:11).
Tunapoangalia Injili nne zinavyomtambulisha Yesu, zile za kwanza tatu kila moja inamweka Yesu katika hali ya historia. Mathayo anaanza na orodha ndefu ya vizazi, na anamuunganisha Yesu na Mfalme Daudi na kumrudia Ibrahimu. Marko anamtambulisha Yesu kupitia kwa mahubiri ya Yohana Mbatizaji. Luka anakwenda mbali kidogo nyuma na Elizabeti na Zakaria na utabiri wa kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji. Lakini Yohana ni wa kipekee katika kumtambulisha Yesu kwetu. Anatupeleka nyuma mbali iwezekanavyo sisi kufikiri. Mwanzo, kabla ya uumbaji wa dunia: ‘Hapo mwanzo kulikuwapo Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.’
Yohana anatupeleka nyuma kupita uumbaji kutukumbusha kwamba Yesu amekuwa Mungu Mwana kutoka milele, kwamba alikuwepo hata kabla ya kuzaliwa kwake, na kwamba anafanana na Mungu Baba.
Twamwona Yesu kama Neno la Milele, aliyekuwako toka mwanzo, sio kwa sababu alikuwa na mwanzo kama kiumbe, bali kwa sababu yeye ni wa milele. Yeye ni Mungu naye ni Mungu pamoja nasi. Katika Yohana 8:58, Yohana anarekodi maneno ya Yesu mwenyewe; ‘Kabla ya Ibrahimu kuwepo, Nilikuwepo.’
Neno la Milele, aliyekuwa na Mungu naye alikuwa Mungu, alichagua kuingia katika dunia yetu kama mtoto asiyejiweza. Yeye, Neno, alisema na dunia ikawepo. Alikuja kuishi kati yetu ili awe mmoja wetu.
Na kwa hiyo, tunaposafiri katika Ujio, ni nini ambacho Yesu, ambaye ni Neno aliyesema tu dunia ikaumbika, anaweza kusema katika maisha yako katika majira haya?
-
Mpendwa Mungu, tunaingia katika majira haya ya Ujio tukisubiri kusherehekea ujio wa Mwanao wa milele duniani kwetu. Tunasimama tukiwa tunashangazwa na wewe. Tunakushukuru, Yesu, uliye - Mimi Ndiye, Alfa na Omega, kwa ajili ya upendo wako usio na masharti na kwa kuja kuishi pamoja nasi. Tusogeze karibu nawe majira haya ya Ujio. Twaomba tujazwe kuabudu na sifa kwako Krismasi hii tunaposherehekea upendo wako wa milele kwetu.
Amina.
Kuhusu Mpango huu
Tunapoingia Ujio, tukisubiri na kujiandaa kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu, tukiiandaa mioyo yetu kwa ajili ya Krismasi, maneno ya Mtakatifu Yohana yanatutangazia hali ya uungu na uwepo wa milele wa Yesu, aliyekuja ‘kusimamisha hema lake’ kati yetu.
More
Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org