Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tabia Za KiunguMfano

Tabia Za Kiungu

SIKU 3 YA 4

Tabia ya Kimungu katika Kuridhika

Tunaishi enzi ya utumiaji wa bidhaa na hii inaonekana kuwa jambo la kawaida. Watu wanahisi kushinikizwa kubadili chapa ya hivi punde ya mashine au gari. Tamaa ya mara kwa mara ya kupata zaidi inakuwa isiyoweza kuzimika. Ingawa tamaa na kufuatia mambo hayo si dhambi, Wakristo wanapaswa kuchunguza mkao wa mioyo yao. Tuanagzie vile maandiko yanafundisha kuhusu mada hii.

Tabia ya Kimungu katika Kuridhika- ni imani ya ndani kwa ukuu na wema wa Mungu ambayo huzaa matunda ya furaha, amani na shukrani katika maisha ya mwamini.

Kutosheka kwa kimungu ni kupitia kujifunza: Paulo alikuwa amejifunza kuridhika si tu mambo makubwa yalipokuwa yakitukia bali katika kila hali. Alijua jinsi ya kupunguzwa na jinsi ya kuwa na wingi. Huu ndio mtazamo wa kuridhika kwa Kikristo, ambao haubadiliki na mabadiliko ya hali. Mtu anayefurahi katika Bwana nyakati zote. Je, hili si jambo la kutamanika kufuatwa?

Kutosheka kwa kimungu ni matokeo ya kuunganishwa na Kristo: Paulo anasema kwamba siri ya kutosheka kwake ni kwa njia ya Kristo anayemtia nguvu. Ni Mungu anayefanya kazi kwa nguvu sana ndani yake ndiye anayemridhisha katika kila hali. Utoshelevu wa kweli katika maisha haya hautapatikana mbali na muungano katika Kristo. Waumini wanaweza kufuata utoshelevu wa kimungu kwa sababu tunajua kwa ufahamu kwamba Kristo hutuimarisha katika kila njia.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Tabia Za Kiungu

Waumini wameitwa kumwiga Yesu Kristo kwa njia nyingi. Tunachunguza tabia tatu za Kimungu ambazo waumini wanapaswa kujitahidi kukumbatia.

More

Tungependa kumshukuru iServe Africa kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://utumishi.net/