Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tabia Za KiunguMfano

Tabia Za Kiungu

SIKU 1 YA 4

Tabia ya Kiungu ya Upendo

Ulimwengu leo ​​umepotosha maoni yetu kuhusu upendo kwa kuupunguza kuwa hisia. Jamii inayotuzunguka imetufanya tufikiri kwamba tunaweza kumpenda yeyote tunayemtaka na jinsi tunavyotaka. Tutaangazia jinsi maandiko inazungumzia hii mada.

Tabia ya Mungu ya Upendo

Mungu anaelezewa kama upendo na kama mwanzilishi wa yote yaliyo katika upendo. Ikiwa Mungu ni upendo basi hakuna chochote ambacho Mungu amewahi kufanya, anachofanya, au atakachofanya ni cha kutengwa na upendo wake. Mungu alionyesha upendo huu kwa kumtuma mwanawe wa pekee Yesu Kristo kuwa dhabihu ya dhambi zetu. Huu ni upendo mkuu, usio na ubinafsi, uliobeba matusi yote, aibu na fedheha ili kuleta upatanisho kati ya mwanadamu na Mungu. Hivyo twaona upendo wa kibibilia ni ule hutoa kwa moyo mkunjufu.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Tabia Za Kiungu

Waumini wameitwa kumwiga Yesu Kristo kwa njia nyingi. Tunachunguza tabia tatu za Kimungu ambazo waumini wanapaswa kujitahidi kukumbatia.

More

Tungependa kumshukuru iServe Africa kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://utumishi.net/