Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 10/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 10/2024

SIKU 3 YA 31

Kila kitu kwenye ibada ya agano la Sinai kilikuwa na maana yake kiimani. Kwa mfano, kinara cha taa kilidhihirisha uwepo wa Mungu, sanduku la agano ni kiti chake cha kutawala kwa haki, wakati kiti cha rehema kilishuhudia nia yake ya kutusamehe. Lakini kiti hicho kilikuwepo ndani yahema ya pili(m.7), yaani sehemuya ndaniya hema ya ibada, na njia ya kuingia hapo ilikuwa imefungwa kwa pazia kubwa asiingie mtu isipokuwa kuhani mkuu. Maana yake ya kiroho imefafanuliwa katika m.7-8:Katika hema hiyo ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, mara moja kila mwaka; wala si pasipo damu, atoayo kwa ajili ya nafsi yake na kwa dhambi za kutokujua za hao watu. Roho Mtakatifu akionyesha neno hili, ya kwamba njia ya kupaingia patakatifu ilikuwa haijadhihirishwa bado, hapo hema ya kwanza ilipokuwa ingali ikisimama.Yesu alipokufa, tunasoma katika Mk 15:38 kwambapazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini.Tafakari jinsi pazia lilivyopasuka. Inadhihirisha nini kuhusu maana ya kifo cha Yesu na njia yetu ya kumkaribia Mungu?

Andiko

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 10/2024

Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz