Mambo yote ni mapyaMfano
Kumbuka Paulo alieleza kwa Wakorintho kwamba kuahirisha safari yake ilitoka kwenye moyo wa dhati.
Moyo wa dhati ni sifa ambayo imepotea nyakati hizi, ikigubikwa na udanganyifu, kufunika ukweli, majibu makali, uongo, na kujipendekeza. Mwili wa Kristo ungekuwa tajiri kiasi gani kama tungekuwa wasafi na dhati kila mmoja kwa mwenzake, na wale wa ulimwenguni?
Tunaweza kwa makusudi kutokuwaambia watu ndiyo wakati tunamaanisha hapana, au kusema hapana wakati tunamaanisha ndiyo, lakini tunafanya kwa njia ya hila.
Kama tungesimama hapa tungekuwa na some la kutusaidia katika uadilifu na ukweli. Lakini Paulo ana kitu cha ziada zaidi ya kupandisha kiwango chetu cha uadilifu.
Tofauti ya imani ya kikristo siyo tuu kufanikiwa katika viwango vya uadilifu au kuonekana kama mkristo mwenye tabia njema kwa ajili ya kuwa watu wazuri. Paulo tayari alikuwa ametumia muda wake mwingi katika kutafuta hilo, akifanikiwa katika elimu ya kiyahudi, akiwa mjumbe wa mafarisayo, akifundishwa na waalimu maarufu, na akijihesabia haki pasipo dosari. Lakini alitambua "uzuri wake wote" haukuwa kitu bali ni mavi (Wafilipi 3:8).
Kwa kuwa sasa anajitetea juu ya vitendo vyake kwa Wakorintho, maana yake ni kwamba kujitetea kwake kwa udanganyifu kungeenda kinyume na moja ya imani yake ya msingi: Mungu ni mwaminifu. Hawezi kudanganya. Hawezi kulikana neno lake. Alifanya ahadi ya agano kuwakomboa watoto wake, na kila ahadi imejumuishwa humo ni "ndiyo" katika Yesu. Na Yesu ni ndiyo ya Mungu kwetu kwa maisha yenye maana na tumaini tunalolitamani (2 Wakorintho1:19-20). Kwa maneno mengine, "Kwa uhusiano kwa [Yesu], kila ahadi ya mwisho ya Mungu hupokea "ndiyo" kama jibu." Kama Mungu si mwongo kwa ndiyo zake na hapana zake, basi, hata Paulo hakuwa hivyo.
Yawezekana moja ya sababu ambazo siku zote zinatufanya tusiwe wa kweli au wawazi kayika mahusiano ni kwa sababu hatujasimama katika "ndiyo" ya Kristo. Najua nimestuka, na wakati mwingine nimedanganya, mazingira kwa sababu nimetaka maisha yangu yawe kama nilivyotaka. Kusimama katika ndiyo au hapana kungeweza kuhatarisha lengo hilo. Lakini napoweza kutumaini uaminifu wa Mungu, tabia yake na utawala wake juu ya maisha yangu, sihitaji kuwa mdanganyifu au mwongo.
Tunapofunga somo letu, ni sehemu gani imekugusa sana?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Katika safari hii kwenye kitabu cha Wakorintho wa pili, mambo yote mapya yanavumbua theologia ya Paulo katika safari ya imani katika ulimwengu huu na wito wa Mungu kwetu kuwa jasiri. Kelly Minter anatusaidia kuelewa jinsi mwenendo wa wakristo unaweza kuonekana unapingana na tabia zetu za asili, lakini inathibitisha kwamba wa milele na bora zaidi kwa nje. Katika siku tano hizi za mpango huu wa masomo, utavumbua vitu kama: jinsi ya kushughulika na mahusiano magumu, kumwamini Mungu na heshima yako, ukisimamisha utambulisho wako katika Kristo, kuelewa kusudi la mateso na upaji wa Mungu ndani yake, na jinsi tunavyotakiwa kuwa nuru ya injili ulimwenguni.
More