Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mambo yote ni mapyaMfano

All Things New

SIKU 3 YA 5

Wakati paulo anazungumza kuhusu mateso ya Kristo yakimwagika katika maisha yetu, anaweza kuwa anamaanisha muingiliano wa mawazo: 1. Mateso kwa sababu ya Kristo. 2. Mateso yaliyoruhusiwa kwetu na Kristo. 3. Mateso yanayohusiana na Kristo. 4. Mateso kama aliyoyastahimili Kristo. [1] Ninachoamini ni muhimu kwetu kukijua ni kwamba kama waamini, tutapata mateso fulani yaliyodhahiri na uhusiano wetu na Kristo. Wakikristo wengi wanateseka mateso makali ulimwenguni kote wakati wengine wanateseka kidogo, lakini bado makali, kwa ajili ya imani yao. Paulo alitambua kuwa kuna uhusiano fulani ambao unafanyika na Kristo nyakati za mateso kwa sababu hakuna ajuaye mateso zaidi yake.

Bado sijakutana na mtu anayefurahia mateso, lakini nimekutana na wengi ambao wamekuwa na uhusiano wa ndani sana na Yesu katikati ya mateso yao. Kuna sehemu fulani za Yesu ambazo huwezi kuzijua katika njia iliyo rahisi, na mara utakapoonja huo ukaribu naye huwezi kubadilishana na njia nyepesi. Zaidi ya kupata uhusiano huo maalum wa karibu na Yesu (Wafilipi 3:10), Pauo anaonesha sababu nyingine kwa nini mateso huleta baraka.

Kila mateso ya Kristo yanapofurika katika maisha yetu kinachofurika kutoka katika maisha yetu ni faraja ya Mungu (2 Wakorintho 1:5). Hii ni ya kushangaza!

Moja kati ya matamko mazuri katika maandiko yotelinapatikana katika mstari wa 4, "atufarijie katika dhiki zetu zote". Tunapodhikika katika magumu, siku zote ni vigumu kuona kitu nje ya maumivu yetu. Lakini tunapata kusudi kubwa katika dhiki zetu tunapotambua kwamba kwa kufanya hivyo tutawafariji na wengine wanaopitia dhiki kama hizo.

Mateso ya Kristo na faraja yake huenda pamoja katika maisha yetu, sambamba. Kama wakristo, hatuwezi kudhikika pasipo faraja ya Kristo, na naamini hatuwezi kujua faraja yeyote nje ya mateso yake. Kama unapitia dhiki, yawezekana mazito usiyowezaa kuyabeba, pata faraja ya Mungu inayokujia kupitia kwa Yesu kuja maishani mwako. Ameahidi kwa kiwango cha dhiki zako. Unapokutana na faraja ya Mungu, utakuwa na shauku ya kufunga vidonda vya mtu mwingine ambaye anapitia dhiki hizo hizo kwa sababu faraja ya Mungu kwa asili hufurika. Utakuwa nayo ya ziada kwa ajili ya wengine.

  
[1] David E. Garland, The New American Commentary, toleo la 29, 2 Wakorintho (Nashville: Broadman & Holman Publishers, 1999) iliyosomwa Agosti 7, 2017 kupitia mywsb.com.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

All Things New

Katika safari hii kwenye kitabu cha Wakorintho wa pili, mambo yote mapya yanavumbua theologia ya Paulo katika safari ya imani katika ulimwengu huu na wito wa Mungu kwetu kuwa jasiri. Kelly Minter anatusaidia kuelewa jinsi mwenendo wa wakristo unaweza kuonekana unapingana na tabia zetu za asili, lakini inathibitisha kwamba wa milele na bora zaidi kwa nje. Katika siku tano hizi za mpango huu wa masomo, utavumbua vitu kama: jinsi ya kushughulika na mahusiano magumu, kumwamini Mungu na heshima yako, ukisimamisha utambulisho wako katika Kristo, kuelewa kusudi la mateso na upaji wa Mungu ndani yake, na jinsi tunavyotakiwa kuwa nuru ya injili ulimwenguni.

More

Tunapenda kuwashukuru LifeWay Women kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: http://www.lifeway.com/allthingsnew