Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mambo yote ni mapyaMfano

All Things New

SIKU 4 YA 5

Kama kuna jambo la kujifunza kuhusu 2 Wakorintho ambalo limenipa mimi changamoto, ni kwamba Paulo hakimbii mahusiano magumu. Tutajifunza zaidi, lakini Wakorintho walikuwa na mambo fulani na Paulo, na kutokuonekana alipoahidi kwamba atarudi tena ilikuwa ni mojawapo. Lakini Paulo kabla hajaanza kujitetea juu ya matendo yake, kwanza anaweka moyo wake sawa kwao.

Kanisa halikuitikia vyema kwa Paulo katika 1 Wakorintho. Mtenda kazi pamoja na Paulo katika huduma yake, Timotheo, aliwatembelea Wakorintho baada ya Paulo waraka ule, akielezea matatizo makubwa--mambo ya maadili, imani potofu, na mapigano kati yao, kwa uchache tuu. Matokeo yake Paulo alisafiri kutoka Efeso kwenda Korintho ili kushughulika mwenyewe ambayo ameilezea katika 2 Wakorintho 2: 1-2 kama "safari ya masikitiko."

Maandiko ya leo yameonesha kwamba Wakorintho walihoji nia ya Paulo ya kutokurudi. Ijapo aliwapenda kwa moyo wote, kundi la watu lililichochea kanisa la Korintho, wakitilia mashaka juu ya ukweli na asili ya kutjitoa kwa Paulo. Naweza kusema hapa, kwangu mimi, hii ilikuwa mbaya. Nachukiwa kutokueleweka, hasa katika hali ambayo nimejinyima, nimejitoa, nimesimama, na kujikana kwa ajili ya mtu. sisemi hili linatokea kwangu mara nyingi, lakini linapotokea nashindana na maamuzi ya aina mbili: 1. Je, namwamini Bwana na heshima yangu, nikiwa na dhamiri safi mbele yake (mstari wa 12)? 2. Naweza kuendelea kuwapenda wale ambao wamenishutumu?

Siku zote haimaanishi vizuri wakati mtu anapokuambia kwamba unajitetea juu ya jambo fulani. Tunaweza kufikiria kwamba jibu pekee lilio bora ni kunyamaza na kutokueleza chochote. (Mithali 9:8 inasema usimkaripie mwenye dharau.) Lakini wakati mwingine kuelezea hatua zetu siyo tuu ni sahihi, lakini ni muhimu kwa mahusiano. Sasa unajuaje kwamba kwamba ujitetee au usijitetee? Hapa kuna kipimo nachotumia: Kama utetezi wangu unasukumwa na kujilinda na umesimamia kwenye kiburi, hasira, hofu, au kujihesabia haki, mara nyingi kutokana na mwili. Wakati, kama kujitetea kwangu kunasukumwa na upendo kwa mtu mwingine na unasimamia katika ufasaha, unyenyekevu, wema, na ukweli, ni kutoka rohoni. Angalia kayika waraka wote kwamba Paulo alikuwa wazi akijitetea, siyo kwa ajili yake mwenyewe, lakini kwa ajili ya upendo kwa Wakorintho. 

Ni hatua gani ya mwanzo unachukua wakati haujaeleweka au umeshukutumiwa kwa makosa? 

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

All Things New

Katika safari hii kwenye kitabu cha Wakorintho wa pili, mambo yote mapya yanavumbua theologia ya Paulo katika safari ya imani katika ulimwengu huu na wito wa Mungu kwetu kuwa jasiri. Kelly Minter anatusaidia kuelewa jinsi mwenendo wa wakristo unaweza kuonekana unapingana na tabia zetu za asili, lakini inathibitisha kwamba wa milele na bora zaidi kwa nje. Katika siku tano hizi za mpango huu wa masomo, utavumbua vitu kama: jinsi ya kushughulika na mahusiano magumu, kumwamini Mungu na heshima yako, ukisimamisha utambulisho wako katika Kristo, kuelewa kusudi la mateso na upaji wa Mungu ndani yake, na jinsi tunavyotakiwa kuwa nuru ya injili ulimwenguni.

More

Tunapenda kuwashukuru LifeWay Women kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: http://www.lifeway.com/allthingsnew