Kueneza Habari Za Yesu Katika Mwaka WaMfano
Huwa tunatoa jawabu lipi tunapoulizwa na watu kumhusu Yesu?
Ikiwa rafiki atakuja kwako kukuuliza kuhusu Yesu, jambo la kwanza utakalomwambia ni lipi? Je, utamwambia Yesu ni rafiki? Mtu wa kihistoria? Kiongozi wa kidini? Pengine utawapa funzo kutoka kwa Biblia.
Ni suala muhimu kujua namna ya kujibu, na pengine kitu ambacho unaweza kufanyia mazoezi sasa hivi kwa sekunde 30 kabla ya kuendelea na mpango. Haya, jaribu.
Katika somo la leo tunaona kwamba wafuasi wa Yesu wameitwa ili wawe mashahidi! Kwenye kiini chake, uinjilisti hauhusu kumpa mtu mafunzo kuhusu sheria za kiroho, au maelezo ya kinadharia ya kidini. Ni kuwatambulisha kwa mtu, mtu wanayeweza kumjua, mtu atakayebadilisha maisha yao milele.
Mungu alipokuwa anataka kuungana kabisa na binadamu, hakutuandikia mahubiri, alikuja kututembelea mwenyewe. Kazi yetu ni kuwa mashahidi wake, kusaidia kila mtu aliye karibu nasi kumjua Mungu, na kufanya maisha yao yabadilishwe na nguvu za upendo na msamaha wake.
Kumbuka, Mungu ni mtu wa kumfahamu, siyo nadharia ya kuielewa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mwito wa kila Mkristo ni kueneza habari za Yesu zenye uwezo wa kubadilisha maisha na jinsi Yesu anavyoweza kumbadilisha kila mtu kikamilifu. Mpango huu wa siku tano unatoa mwongozo halisi kuhusu jinsi unavyoweza kuitikia mwito huu kila siku na uone Yesu akibadili maisha ya walio karibu nawe wanaohitaji kumfahamu.
More
Tungependa kumshukuru YesI kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://yesheis.com/