Kueneza Habari Za Yesu Katika Mwaka WaMfano
Ili tuweze kuubadilisha utamaduni wetu, tunahitaji kuufahamu utamaduni huo
Je, umewahi kujiuliza ni kwa nini Ukristo umenawiri katika baadhi ya mataifa ilhali katika mataifa mengine unakua kwa shida sana? Pengine hii ni kwa sababu kila utamaduni ni tofauti. Tangu pale injili ilipohubiriwa kwa mara ya kwanza katika kitabu cha Matendo, changamoto kwa Wakristo imekuwa ni kuwasilisha injili kwa njia inayoeleweka. Hata leo, hali ni hiyo hiyo, na tumejitwika jukumu la kuelezea mambo ya kweli yanayohusu uzima wa milele kwa njia inayofungamana na utamaduni wa sasa.
Kwenye somo la leo, tunamwona mtume Paulo akizihusisha habari za Yesu na maisha ya kikundi cha watu alichokuwa akizungumzia. Alitumia mawazo waliyoyafahamu na kurejelea vitu walivyovijua, na kisha akatumia imani zao wenyewe kumwelezea Mungu!
Ufanisi wetu katika kueneza habari za Yesu shuleni kwetu, nyumbani, katika janibu zetu, kazini au kanisani kunafungamana moja kwa moja na jinsi tunavyowafahamu wale wanaotuzingira na uwezo wetu wa kuingiliana na wao.
Ili kuuelewa vyema utamaduni wa kimagharibi, yesHEis ilitoa wajibu kwa shirika moja la kiutafiti ili lichunguze na kutoa ripoti kuhusu tabia na mitazamo ya kizazi cha sasa (Gen Y) kuhusu imani na Ukristo. Japo utafiti ulifanywa kule Australia, unaashiria tamaduni nyinginezo nyingi. Matokeo yalionyesha kwamba vijana walio kwenye mtindo wa kisasa wana mazoea ya kushutumu dini katika jamii, asilimia 55% wanadai kwamba dini ina athari mbaya katika jamii. Kinyume chake, wengi wao wana maoni mazuri kuhusu masuala ya kiroho kuliko dini, huku wawili kati ya watatu (64%) wakidai kwamba masuala ya kiroho yana athari nzuri katika jamii.
Huku tukijitahidi kuuelewa utamaduni wetu pamoja na kuwaelewa watu ambao Mungu ameweka karibu nasi, tutapata mbinu bora za kuingiliana nao na kutoa jawabu kuhusiana na maoni hasi na imara waliyo nayo watu wengi dhidi ya dini na Ukristo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mwito wa kila Mkristo ni kueneza habari za Yesu zenye uwezo wa kubadilisha maisha na jinsi Yesu anavyoweza kumbadilisha kila mtu kikamilifu. Mpango huu wa siku tano unatoa mwongozo halisi kuhusu jinsi unavyoweza kuitikia mwito huu kila siku na uone Yesu akibadili maisha ya walio karibu nawe wanaohitaji kumfahamu.
More
Tungependa kumshukuru YesI kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://yesheis.com/