Soma Biblia Kila Siku 04/2024Mfano
Wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni(m.11).Yesu alipoiona imani kubwa kwa mtu ambaye si Mwisraeli, alikumbuka ahadi za Mungu za Agano la Kale, kwa mfano Isa 49:5-6 ilipoandikwa,Alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote. Ahadi hizi zinatabiri kwamba Kristo hatakuwa Mwokozi kwa ajili ya Waisraeli tu, bali kwa ajili ya ulimwengu mzima! Lengo hili likishafikiwa, ndipo Yesu atakuja mara ya pili.Habari njema ya ufalme itahubiriwa katika uliwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja(Mt 24:14). Je, Tanzania nzima imeshafikiwa na Injili?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hosea na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/