Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

SIKU 9 YA 30

Waisraeli kumkataa Kristo kulifanya Mataifa kubarikiwa na utajiri wa Kristo. Kwa mfano tuna habari hizi za kihistoria katika Mdo 13:44-47:Hata sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu. Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana. Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa. Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.Hiyo inamfanya Paulo kuuliza swali katika m.12:Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa Mataifa, je! Si zaidi sana utimilifu wao?Ndipo Paulo anatufunulia siri ya mpango wa Mungu kwamba kweli siku moja wengi wao wataokoka:Sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao(m.25-27; lingutimilifu waokatika m.12)! Haya yatatokea baada ya Injili kuenezwa kwa Mataifa yote (Mt 24:14,Habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja). Na ulimwengu utabarikiwa sana kwa kuokoka kwao.Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho wa ulimwengu, je! Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhai baada ya kufa?(m.15; ling. ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu katika Mwa 12:3,Katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa).

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Warumi na Methali. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/