Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023Mfano

Kuna utaratibu wa namna ya binadamu kutendeana sisi kwa sisi. Mtu wa Mungu anajihadhari na masengenyo, ugomvi na kutokuaminika, maana mambo kama hayo ni hatari kama rungu, upanga au mshale mkali. Mungu pekee ndiye atoaye njia sahihi, bora na kamilifu ya kukabiliana na adui yako. Kristo anatuagiza, “Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi” (Mt 5:44). Neno la Mungu ni hekima inayozingira maisha yako. Tukiwa bila Neno hilo au tusipolifuata, ni sawa na kuwa na mwili usio na kinga.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Warumi na Methali. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/