Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023Mfano
Kuna usemi usemao, “Usitupe kito mbele ya nguruwe” (ling. Mt 7:6,Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua). Mtu mwenye hekima ya Mungu ni kama chombo chenye dira inayoaminika. Hekima ya kimungu hutoa silaha ya kukabiliana na uovu na upumbavu. Kwa mfano, Kristo akiwa mbele ya Pontio Pilato hakujibu kila swali aliloulizwa. Kunyamaza kwake kulionyesha ushindi dhidi ya uovu. Kabla ya kujibu chochote, mtazame Kristo kwanza. Ameahidi kutupa ufasaha wa maneno na hekima tukishtakiwa kwa sababu ya imani yetu:Basi, kusudieni mioyoni mwenu, kutofikiri-fikiri kwanza mtakavyojibu;kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawafisha baadhi yenu.Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu.Walakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu.Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu(Lk 21:14-19).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Warumi na Methali. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/