Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Acha! Usiwe Na Wasiwasi ZaidiMfano

Acha! Usiwe Na Wasiwasi Zaidi

SIKU 6 YA 7

Mungu ndiye Nguvu Kuu

Wengi wetu tunajua jinsi unavyohisi ukiwa peke yako gizani. Ikiwa uliwahi kuchukua takataka nje usiku sana au ukajikuta umekwama kando ya barabara usiku, basi unaelewa - akili yako inaweza kuunda vivuli vilivyofichwa au picha. Kabla hujajua, nywele nyuma ya shingo yako huanza kuinuka.

Walakini, ikiwa utawasha tochi, hofu yako hutoweka haraka kwa sababu nuru hufichua ukweli.

Katika Zaburi ya 23, Daudi aliandika kuhusu wakati ambapo alikuwa na hakika kwamba angepoteza uhai wake. Ulikuwa ni msimu ambapo alitembea “katika bonde la uvuli wa mauti.” (Aya. 4) Hata hivyo, hakuogopa kwa sababu alijua yule aliyetembea naye alikuwa na uwezo wa kuleta nuru kwenye hali ya giza totoro na kubadilisha wasiwasi wake kwa imani.

Unapokumbana na matatizo ya kutisha maishani mwako geukia upendo wa Mungu wenye uhakika na usiokoma milele. Unapoamka katikati ya usiku kwa minong'ono ya uwongo wa adui – jikumbushe kwamba Kristo alishinda na wewe pia utashinda. Tangaza kile unachojua kuwa ni kweli!

Kimsingi, Daudi alisema, “Nijapopita katika tisho la kifo, sitaogopa kwa sababu Bwana na Mwokozi wangu yuko karibu nami.” Mungu ndiye nguvu kuu zaidi na anakupenda kwa upendo wa dhati na wa kibinafsi. Ingawa maisha yanaweza kuwa giza, nuru yake Mungu inaendelea kuangaza. Hakuna giza linaloweza kuzima nuru ya upendo wa Mungu. Hauna sababu ya kuwa na wasiwasi - Mungu yu pamoja nawe!

Ubongo wako unaashiria hatari katika maisha yako iwe ni ya kweli au ya kufikiria tu. Unachohitaji kufanya wakati ishara hizi za wasiwasi zinatokea ni kuzitathmini na kuzijaribu. Tambua iwapo hatari hii ni tishio la kweli au la kimawazo tu. Ikiwa imefikiriwa, basi aichilie iondoke. Ikiwa hakuna hatua unayoweza kuchukua ili kuipunguza - geuza mawazo yako kwa kitu kingine.

Unaweza kushinda vitisho kwa kufanya badilishana wasiwasi hiyo kwa kuamini kwamba Mungu yu pamoja nawe na anadhibiti yote, wala huna haja ya kuogopa. Kama vile Daudi alivyoandika katika Zaburi 34:3 – 5, “Mtukuzeni Bwana pamoja nami, na tuliadhimishe jina lake pamoja. Nilimtafuta Bwana, naye akanijibu, akaniokoa na hofu zangu zote. Walimtazama na kung’aa, na nyuso zao hazitaaibika kamwe.”

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Acha! Usiwe Na Wasiwasi Zaidi

Je! unajua Yesu anasema nini kuhusu wasiwasi wetu? Acha. Ndiyo, anatuambia tuiache. Wasiwasi ni moja ya dalili kuu kwamba imani yetu imetikisika na imani yetu iko chini. Wakati wewe au mimi tunakuwa na wasiwasi, tunakosa kuweka imani ifaayo juu ya udhibiti mkuu wa Mungu. Bado sote, bado tunafanya hivyo, sivyo? Ndiyo maana Tony Evans ameweka pamoja mpango wa kusoma wa siku 7 ili kukusaidia WEWE kushinda wasiwasi. Unaweza kuvunja mzunguko na kubadilishana wasiwasi kwa amani.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative