Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Acha! Usiwe Na Wasiwasi ZaidiMfano

Acha! Usiwe Na Wasiwasi Zaidi

SIKU 2 YA 7

Haina Haja ya Kuwa na wasiwasi

Jambo la kwanza ambalo Yesu anataka tutambue kutokana na kifungu tulichotazama jana (Mathayo 6:25 – 26) ni kwamba ikiwa tumefungwa na ngome ya kihisia ya wasiwasi, tumesahau Baba yetu ni nani. Anasema Baba yetu wa mbinguni anatuona kuwa wa thamani zaidi kuliko ndege na maua. Anatanguliza sehemu hii inayohusu wasiwasi kwa kusema katika aya ya 25, “Kwa sababu hii.” Kwa sababu gani? Katika aya ya 24 inasema, “Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.” Ikiwa pesa ni bwana wako, utajikuta unahangaika nayo na haumtumikii Mungu. Yesu alionyesha picha kamili jinsi wasiwasi ilivyo alipouliza, “Ni nani kati yenu kwa kuhangaika anaweza kuongeza saa moja kwenye maisha yake?” (Mathayo 6:27) Tukifanya yote tuwezayo na kisha kumkabidhi Mungu matokeo, basi haina maana kuwa na wasiwasi.

Watu wa Mungu wanaomjua na kuna uhusiano kati yake nao, hawapaswi kuishi au kufikiri sawa na wale wasiomjua. Mungu anatukanwa kutokana na wasiwasi wetu; nayo inazuia uwezo wetu wa utendaji kama watoto wake wamwaminio.

Mimi na Lois tuna sehemu ya kutorokea kutoka kwa shamrashamra za maisha ya jiji. Ninapoamka asubuhi huko, huwa kila mara nasikia ndege wakiimba nje ya dirisha langu wakiwa wamejawa na amani na furaha kwa sababu hawana wasiwasi. Hawa ni ndege wasio na akaunti ya benki, fedha za kuezeka kwa pamoja, na hawana njia za kazi. Wanaelewa kwamba yule aliyewaumba amewapa mahitaji yao yote.

Mungu huwalisha ndege lakini hawana thamani ya milele kwake. Lakini una thamani kubwa sana kwake hata akamtoa mwanawe wa pekee kununua wokovu wako na ukombozi kutoka kuzimu.

Huenda ulilelewa katika mazingira ambayo mahitaji yako hayakutimizwa huku mahitaji ya wale walio karibu nawe yakizingatiwa. Au uliwahi salitiwa katika uhusiano wa karibu – labda ndoa na yote hayo yanaibua hisia za wasiwasi, hofu na shaka. Yesu anazungumza kuhusu Baba yako wa “mbinguni,” si watu wengine ambao wanaweza kukusahau au kukuacha. Unapofanya kutofautisha hilo katika akili yako na katika mawazo yako, kwamba Mungu si kama wengine - utakuwa kwenye njia yako ya kushinda wasiwasi.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Acha! Usiwe Na Wasiwasi Zaidi

Je! unajua Yesu anasema nini kuhusu wasiwasi wetu? Acha. Ndiyo, anatuambia tuiache. Wasiwasi ni moja ya dalili kuu kwamba imani yetu imetikisika na imani yetu iko chini. Wakati wewe au mimi tunakuwa na wasiwasi, tunakosa kuweka imani ifaayo juu ya udhibiti mkuu wa Mungu. Bado sote, bado tunafanya hivyo, sivyo? Ndiyo maana Tony Evans ameweka pamoja mpango wa kusoma wa siku 7 ili kukusaidia WEWE kushinda wasiwasi. Unaweza kuvunja mzunguko na kubadilishana wasiwasi kwa amani.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative