Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Acha! Usiwe Na Wasiwasi ZaidiMfano

Acha! Usiwe Na Wasiwasi Zaidi

SIKU 5 YA 7

Haiwi bora kuliko hivi

Hadithi ya Hana ni mojawapo ya hadithi ambayo wengi wetu tunaweza kujihusisha nayo. Tuko katika hali ngumu, bado na licha ya maombi yetu ya kudumu, hali haiwi bora. Hana alikuwa mmoja wa wake wawili wa Elkana na hakuweza kupata watoto, lakini Penina, mke mwengine, angeweza. Katika utamaduni wa kibiblia, kuzaa watoto kwa mwanamke ilikuwa muhimu kwa sababu wao ndio wangekutunza. Kwa hiyo, Hana hakubeba aibu na maumivu yake ya ndani tu, bali Penina ‘alimchokoza sana ili kumkasirisha. (1 Samweli 1:6)

Maumivu ya Hana yalimfanya atokwe na machozi – kiasi kwamba alishutumiwa kuwa mlevi hekaluni alipokuwa akimlilia Mungu kwa ajili ya mtoto!

Safari ya Hana na Elkana ya kila mwaka ya Shilo kwenda kutoa dhabihu kwa Bwana ilikuwa ni siku yake ya huzuni zaidi. Alimwabudu Bwana ingawa tatizo lake la kudumu lilimtia wasiwasi na kumfadhaisha. Angetazama wale walio karibu naye wakifurahia watoto wao na kupumzika kwa usalama katika maisha yao ya baadaye kutokana na udhamini wa wana wao.

Ninashuku umekuwa katika hali kama hii pia. Tatizo halikuwa kwamba hali ilizidi kuwa mbaya – hakuna kilichobadilika kwa Hana. Yaelekea mashaka yaliingia kichwani mwake ikiwa mume wake angeendelea kumpenda.

Je, unaweza kufahamu jinsi Hana alihisi? Ingawa hali yake haikubadilika aliweka imani, tumaini na matarajio katika Mungu.

Jambo la maana katika hadithi hii ni kwamba Hana alivumilia mwaka baada ya mwaka –

kushinda wasiwasi wake kupitia sala na ibada. Mungu alijua uchungu wake na ukimya wake haupaswi kuonekana kama kutojali au kutohusika.

Mungu alikuwa akimleta Hana katika kiwango ambapo alikuwa tayari kumrudishia Mungu kitu ambacho alikuwa akitaka zaidi - mwanawe Samweli. Mungu alikuwa na mpango maalum kwa ajili yake – kuwa nabii mkuu. Njia pekee ambayo Hana angehamishwa hadi mahali hapa pa kujisalimisha ilikuwa kupitia kwa utasa wake wenye uchungu. Hana alimuahidi Bwana kwamba angempa Samweli ikiwa angefungua tumbo lake la uzazi. Alitimiza kiapo chake alichoweka na Mungu akambariki Hana na watoto wengine watano. (1 Samweli 2:21)

Rafiki, ikiwa kuna jambo fulani maalum ambalo una wasiwasi nalo - fikiria kumwendea Bwana na kwa hiari kuliacha au umrudishie. Mara nyingi, Yeye anakungoja wewe umtumaini kabla hajaingilia kati na kutenda jambo kwa niaba yako. Ni muhimu sana kwake kutimiza kusudi na mpango wake maishani mwako kuliko kutimiza matakwa yako.

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Acha! Usiwe Na Wasiwasi Zaidi

Je! unajua Yesu anasema nini kuhusu wasiwasi wetu? Acha. Ndiyo, anatuambia tuiache. Wasiwasi ni moja ya dalili kuu kwamba imani yetu imetikisika na imani yetu iko chini. Wakati wewe au mimi tunakuwa na wasiwasi, tunakosa kuweka imani ifaayo juu ya udhibiti mkuu wa Mungu. Bado sote, bado tunafanya hivyo, sivyo? Ndiyo maana Tony Evans ameweka pamoja mpango wa kusoma wa siku 7 ili kukusaidia WEWE kushinda wasiwasi. Unaweza kuvunja mzunguko na kubadilishana wasiwasi kwa amani.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative