Yesu Mwalimu WetuMfano
Tunapoingia kwenye sebule na kuona kila mtu ameketi isipokuwa mtu mmoja, kwa kawaida hudhani kuwa yule aliyesimama ndiye yu kwenye usukani. Anazungumza, anafundisha, au ndiye mwenye udhibiti wa chumba kile – angalau kwa muda huo. Kushawishi au kuzungumza kwa kiwango chochote cha mamlaka, kwa kawaida huwa tunasimama ili husimama iliyo tuonekana kana kwamba tumechukua udhibiti wa mkutano.
Watu wa Kiyahudi kwenye Agano Jipya, hata hivyo, walikuwa na mwelekeo tofauti. Katika desturi ya Kirabi, mwalimu aliketi alipokuwa akizungumza. Tunaona hili mara nyingi Yesu akifanya hivyo, yule Rabi wa kuhama hama, iwe alikuwa kwenye sinagogi au la. Katika Luka 4:20, baada ya Yesu kusoma maandiko, aliketi chini na kuzungumza. Hotuba ya Yesu ya mlimani yaanza hivi: “Naye alipowaona makutano, alipanda mlimani, na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia; akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema.” (Mathayo 5: 1 – 2). Kufunza wakati ambapo umeketi ilikuwa kufunza kutoka kwenye kiwango cha mamlaka.
Marko katika ubeti wetu, hakusema kwamba Yesu alikuwa ameketi, ila jambo moja ni wazi; wale waliomsikilizia akifunza walijua alifanya hivyo kwa mamlaka. “Wakashangaa mno kwa mafundisho yake. Kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi.”
Kwa sisi wengine, mamlaka yoyote tuliyo nayo ina mipaka kwa majukumu ambayo tumepewa. Iwe wewe ni rais wa Marekani au mama anayeshughulikia mtoto wa miaka mitatu, mamlaka yako yafikia kiwango fulani tu. Ina mwisho wake, ni ya dunia. Lakini, mamlaka ya Yesu, haina kikomo kwa sababu kihalisia inakaa ndani mwake. Alifunza kwa mamlaka si kama ya mwingine yeyote kwa sababu Yeye Mwenyewe ndiye mamlaka hiyo. Anajumuisha ukweli kamili. Alisema “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima” (Yohana 14:6).
Yesu pia aliunga mkono mamlaka yake kwa matendo yake. Alidhihirisha utegemezi wa maneno yake iliyoandamana kwa miujiza.
- Alilipa kodi yake kwa sarafu kutoka katika kinywa cha samaki (Mt. 17:24 – 27).
- Alitoa pepo wanafunzi wake hawakuweza (Marko 1:23 – 27).
- Alifufua wafu (Marko 5:35 – 42).
- Aligeuza samaki wachache na mikate kuwa chakula kikubwa cha maelfu (Marko 6:30 – 44).
- Alitembea juu ya maji, wafuasi wake walihofu (6:45 – 52)
Matendo yake na miujiza ilifanya maneno yake yasadikike. Iwapo mafundisho ya Yesu hayangeenda mbali zaidi ya wale waliomsikia mwanzoni akisema, mamlaka yaliyokuwamo katika mafundisho yake yangeweza kupotea kwenye rafu zenye vumbi za historia. Lakini mafundisho yake hayakuishia na matukio hayo. Kwa kweli, muda mfupi kabla ya kurudi kwa Baba yake, Yesu aliwaamuru wafuasi wake waende ulimwenguni na kufundisha kwa niaba yake. Kutokana na mamlaka yake, ametupa agizo hili. Zaidi ya hayo, baada ya yeye kutoa agizo hili, alirudi mbinguni na, kwa mara nyingine tena, akaketi. Akaketi kwenye mkono wa kuume wa Mungu (Marko 16:19).
Yesu ameketi katika nafasi ya mamlaka leo, na ametuita sisi kuishi na kufundisha maneno yake kutoka kwenye nafasi ya mamlaka.
Kuhusu Mpango huu
Wewe unaenda wapi kujifunza jinsi ya kuwa mtu bora au kushinda changamoto? Wewe unamtafuta nani akufunze lilo bora au jinsi ya kufanya maamuzi sahihi? Je! Unakwenda kwenye magazeti? Mtandao wa kijamii ya YouTube? Tony Evans anashiriki kuhusu Mtu Mkuu zaidi jinsi aweza kukufundisha kuhusu maisha naye ni Yesu Kristo. Hebu tuchunguze jinsi Mpaji wa uzima pia ni Mwalimu wa maisha.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/