Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yesu Mwalimu WetuMfano

Yesu Mwalimu Wetu

SIKU 2 YA 3

Wayahudi wengi wa siku hiyo wangefikiri kwamba njia ya uzima wa milele ilikuwa kupitia utii kwa sheria. Lakini mtu mmoja alimjia Yesu mbio, akitaka kujua, “Mwalimu Mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?” Hatujui alichokuwa amesikia hapo awali, lakini jambo fulani katika mafundisho ya Yesu (na pengine mamlaka ya mafundisho hayo) lilimsadikisha kwamba licha ya jitihada zake alikuwa amekosa kitu.

Huenda mwanamume huyo hata alikuwa akikubali chanzo cha mafundisho na mamlaka ya Yesu kwa kumwita “Mwalimu Mwema.” Kwa Wayahudi, Mungu ni mwema kimsingi (1 Nya. 16:34); kwa kweli, kwa kuwa wema wa Mungu ulikuwa mkuu zaidi kwao, hawakumtaja mtu mwingine yeyote kuwa mwema. Swali la Yesu, “Kwa nini kuniita mwema?” haikuwa kupinga wazo la mtu huyo la kumwita mwema, lakini badala yake ilikuwa kumwongoza mtu huyo kutafakari umuhimu wa kile alichokuwa akisema. Ikiwa Mungu ni mwema, na Yesu ni mwema, basi Yesu ni Mungu.

Kana kwamba anakaribia kuunga mkono wazo la Kiyahudi kwamba utii kwa sheria huleta uzima wa milele, Yesu aliorodhesha baadhi ya Amri Kumi (Kut. 20:1 – 16). Yesu alianza pale mtu huyo alipokuwa—kujitahidi kupata uzima wa milele kwa kushika sheria—lakini angemwonyesha mtu huyo kwamba haitoshi. Mtu huyo alikubali utiifu wake haraka, lakini Yesu alimwitia mtu huyo kwa kiwango cha juu zaidi cha utii, zaidi ya kushika tu maandishi ya sheria.

Ni nini “kitu kimoja” ambacho mtu huyo alikosa? Alikuwa na upungufu wa imani kali kwa Mungu ambayo ingemruhusu kuacha kila kitu na kumfuata Yesu. Angeweza kuonyesha kujitoa kwake kwa Mungu kwa kuwa na huruma zaidi kwa wahitaji kuliko kupenda mali yake.

Kwa wengine, maneno hayo yanaweza kusikika kuwa makali. Lakini tusisahau kwa nini Yesu alisema nao: “Akimtazama, Yesu alimpenda.” Upendo wa Yesu uliendesha kila kitu alichosema na kufanya, ikijumuisha mafundisho yake. Yesu wa Biblia sio mwigizaji asiyejali wa Ulaya mwenye duara ya mwangaza imemzunguka kichwani, mwenye lafudhi ya Uingereza ambayo tumetazama mara kwa mara kwenye sinema. Yeye si, masihi asiyekuwa na kina, aliyechorwa kwenye ubao wa flana. Bwana wetu alihisi huruma kubwa, na huruma hiyo ilichochea matendo yake ya dhabihu yaliyofanywa kwa upendo.

  • “Alipoona umati, akawahurumia …” (Mt. 9:36)
  • “Alipokuwa akishuka pwani, aliona umati mkubwa wa watu, akawaonea huruma …” (Mt. 14:14)
  • “Yesu akawahurumia, akayagusa macho yao.” (Mt. 20:34)
  • “Yesu akamwonea huruma, akanyoosha mkono wake…” (Marko 1:41)
  • “Bwana alipomwona, alimhurumia …” (Luka 7:13)
  • “Alipofika karibu aliuona mji, akulilia aliulilia…” (Luka 19:41)

Kwa upendo wake, Yesu alithibitisha matendo ya mtu huyu na kumpa kipande kimoja chenye nguvu sana cha ushauri: Auze vyote alivyokuwa navyo na awape maskini. Kwa sababu, kwa kufanya hivyo, angeweka hazina mbinguni.

Kutokana na upendo wake, Yesu aliwasilisha kwa mtu huyu—na sisi! — ukweli unaolipuka, uhalisi wa ajabu ambao unapaswa kuongoza yote tunayofanya. Maisha haihusu tu kile tunachoweza kuona, kusikia, kuonja, kugusa, na kunusa. Maisha yanaenda zaidi ya tunavyojua sasa. Hazina mbinguni ni za thamani zaidi kuliko vyumba vya kuhifadhi vilivyojaa vitu.

Kwa upendo wake, Yesu alimhimiza mtu huyo aache mambo yote yaliyokuwa yakimzuia asipate hazina ya kweli.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Yesu Mwalimu Wetu

Wewe unaenda wapi kujifunza jinsi ya kuwa mtu bora au kushinda changamoto? Wewe unamtafuta nani akufunze lilo bora au jinsi ya kufanya maamuzi sahihi? Je! Unakwenda kwenye magazeti? Mtandao wa kijamii ya YouTube? Tony Evans anashiriki kuhusu Mtu Mkuu zaidi jinsi aweza kukufundisha kuhusu maisha naye ni Yesu Kristo. Hebu tuchunguze jinsi Mpaji wa uzima pia ni Mwalimu wa maisha.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/