Kufuata AmaniMfano
Kuwa katika Amani na Yaliyopo
Utahisi kana kwamba ni mbadiliko wa ghafla kuanza kila siku kwa kukumbuka upendo, huruma na uaminifu wa Mungu. Hata ingawa una kazi nyingi ya kufanya, ni muhimu utenge wakati, unaweza kuwa asubuhi na mapema au jioni, kumwuliza Mungu akupe zawadi ya amani.
Methali ya Kiafrika:
Unyamavu unaleta amani ambayo huleta usalama. ~ Methali kutoka Afrika Mashariki
Mathayo 5:9 inasema, “Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu.”
Baraka kuu, tunapopokea zawadi hii, si kujiwekea bali ni kuwapa wengine. Tunafaa kuwa wenye kuleta amani kwani dunia hii inahitaji amani. Tunafanya hivi kwa kuombea wengine wawe na amani, kuombea amani popote ambapo pana vita, kuombea viongozi na wanaoleta amani katika nchi zenye vita wawe na hekima na utambuzi wa mambo.
Methali ya Kiafrika:
Haraka, haraka haizui kifo wala kuenda polepole haizui uhai. ~ Methali ya Kiibo
Kanisa linafaa kuwa ishara hai na kushuhudia uponyaji, upatanisho na urejesho wa Kristo. Tearfund ina mradi unaoitwa Rhythms ambao una vitendo vingi unaweza kufanya ili uzidi kutii Kristo kwa kuleta amani hata katika maisha yako ya kawaida.
Tendo:
Enda uangalie watu. Ombea hata watu usiowajua kwani Mungu anawajua. Omba kwamba wataweza kujua upendo wa Mungu na kwamba Mungu atawazunguka katika hali zote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Tearfund inatafuta uongozi wa Mungu ili iwe sauti ya nguvu juu ya amani, mahusiano kurudishwa, na upatanifu kati ya jumuiya mbalimbali katika dunia. Somo hili la siku 7 lina matendo ya kila siku ili urudishe mahusiano yako na wengine na uombee dunia tunayoishi. Somo hili linatumia hekima kutoka methali za Afrika kutusaidia kufunua amani ya kweli ya Mungu.
More