Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kufuata AmaniMfano

Pursuing Peace

SIKU 3 YA 7

Amani na Wengine

Katika makanisa mengine kuna tendo linaloitwa kutakiana amani linaloashiria upendo na umoja wa kikristo ukigawanywa miongoni mwa waumini. Tunapozoea kufuata tamaduni, ni rahisi kusahau umuhimu wake. Jamii bora ni ile iliyo katika amani na kueneza hii amani kwa watu wengine. Inaonekana vigumu kuonyesha amani na upendo kwa watu tusiowajua kwani ubinafsi umeongezeka katika jamii.

Kutakia wengine amani inaweza kuwa kumtembelea jirani mzee, kumpa mtu maji ya kunywa, kulisha maskini ama kuchunga mtoto. Aidha, inaweza kuwa kumsamehe aliyekukosea, kuwatetea wanyonge, kuendelea kutembea kilomita nyingine ingawa umechoka, ama kuomba radhi. Lazima maombi yaandamane matendo haya. Tuombee amani ya kweli na Ufalme wa Mungu ujengwe duniani.

Methali za Kiafrika:

Iwapo kuna amani, kiongozi habebi ngao. ~ Methali ya Kiganda

Mfalme akiwa na washauri wazuri, enzi yake itakuwa ya amani. ~ Methali ya Kiashanti

Tearfund inaleta amani na mabadiliko katika jamii. Soma hadithi hii kuhusu mshiriki wa Tearfund ambaye ameweza kuwasaidia wanajamii katika Nijeria kuwacha kuchukiana.

Tendo:

Je, kuna mtu ambaye unafaa kupatana naye? Panga kukutana naya na umweleze sababu ya mkutano huo. Mwombe Mungu akuonyeshe jinsi ya kumpa upendo na msamaha wa Kristo.

Andiko

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Pursuing Peace

Tearfund inatafuta uongozi wa Mungu ili iwe sauti ya nguvu juu ya amani, mahusiano kurudishwa, na upatanifu kati ya jumuiya mbalimbali katika dunia. Somo hili la siku 7 lina matendo ya kila siku ili urudishe mahusiano yako na wengine na uombee dunia tunayoishi. Somo hili linatumia hekima kutoka methali za Afrika kutusaidia kufunua amani ya kweli ya Mungu.

More

Tungependa kushukuru Tearfund kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.tearfund.org/yv