Kufuata AmaniMfano
Kupatana na Yaliyopita
Kupatana na yaliyopita ni vigumu kama vile maamuzi unayojuta ama kusamehe aliyekukosea. Ni muhimu kushughulikia na yaliyopita ili isidhuru yaliyopo au yajao. Tafakari kupanda baiskeli. Iwapo utatazama nyuma, au kuangalia chini, hakika utagonga kitu. Ni muhimu uzidi kuendelea kutazama mbele na kushiriki katika mambo mapya ambayo Mungu anafanya.
Njia muhimu ya kupatana na yaliyopita ni kuchagua msamaha. Unaposamehe aliyekukosea, si kwamba unakubali kwamba yaliyotendeka ni mema bali unajipa ruhusa kusonga mbele na maisha yako. Yaliyopita ni mazuri kwa sababu ya mambo mawili: kukufunza na kufurahia maisha Mungu amekupa.
Methali ya Kiafrika
Iwapo kuna amani, kiongozi habebi ngao . ~ Methali ya Kiganda
Tearfund inashiriki katika kuleta amani na upatanisho. Kuna hadithi moja hapa kutoka Rwanda kuhusu jinsi msamaha unaweza kuponya hata vidonda sugu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Tearfund inatafuta uongozi wa Mungu ili iwe sauti ya nguvu juu ya amani, mahusiano kurudishwa, na upatanifu kati ya jumuiya mbalimbali katika dunia. Somo hili la siku 7 lina matendo ya kila siku ili urudishe mahusiano yako na wengine na uombee dunia tunayoishi. Somo hili linatumia hekima kutoka methali za Afrika kutusaidia kufunua amani ya kweli ya Mungu.
More