Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano
Wakamwinamia mpaka nchi ... wakainama, wakasujudu (m.26 na 28). Hapa twaona jinsi ndoto ya ujana wake Yusufu inavyotimia. Kwa kulinganisha na 37:5-8 utaona kuwa Yusufu aliota ndoto, akawapa ndugu zake habari, ... akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu. Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Kumbe, ndoto yake Yusufu wakati ule ilitoka kwa uweza wa Mungu! Hakuitunga yeye mwenyewe, bali ilikuwa unabii wa kweli! Yusufu alipowaketisha mezani alifuata umri wao sawasawa, wakastaajabu wao kwa wao (m.33). Huenda hapo walianza kujisikia kutambuliwa. Pia alimpa Benyamini chakula kingi kuliko wao. Labda alitaka kuona kama watamwonea wivu kama walivyomwonea yeye.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/