Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022

SIKU 7 YA 30

Watu hawa watakula pamoja nami adhuhuri (m.16). "Adhuhuri" = "mchana”. Kwa Wayahudi kula pamoja ni dalili ya kupatana na kupendana. Mara Yusufu alipoona kwamba wamemleta Benyamini akaanza kuwaandalia chakula. Maana sasa alijua hakika wamesema ukweli. Tena alifurahi mno kumwona mdogo wake (m.30, moyo wake ulimwonea shauku nduguye). Ila ndugu zake hawakujua sababu ya kupelekwa nyumbani mwake. Kwa hiyo waliogopa kutokana na zile fedha walizorudishiwa (m.18). Lakini walipomkaribia mtumishi wa Yusufu ili kumwambia wasiwasi wao, akawatulia vizuri, akawaambia, Amani iwe kwenu, msiogope; Mungu wenu, naye ni Mungu wa baba yenu, amewapa akiba katika magunia yenu; fedha zenu ziliniwasilia (m.19 na 23)!

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/