Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano
Fanyeni haraka, mmwendee baba yangu, mkamwambie, Hivi ndivyo asemavyo mwanao Yusufu, Mungu ameniweka kuwa bwana katika Misri yote, basi unishukie, usikawie (m.9). Leo sisi twajifunza mambo mawili kutoka kwa Yusufu: 1. Bado ni mcha Mungu. Yaani baada ya kupata mamlaka na cheo hakujivuna, bali aliendelea kumpa Mungu utukufu (m.5, Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu)! 2. Alikuwa mwaminifu kwa baba yake na ndugu zake (katika m.10-11 anamwambia babaye, Utakaa katika nchi ya Gosheni, utakuwa karibu nami, wewe, na wanao ... usije ukaingia katika uhitaji). Yusufu alikuwa hajawasahau. Bado aliwapenda sana. Tena alikuwa amewasamehe. Inaonekana katika anavyowaambia katika m.5-8, Msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu. Maana miaka hii miwili njaa imekuwa katika nchi, na iko tena miaka mitano isiyo na kulima wala kuvuna. Mungu alinipeleka mbele yenu kuwahifadhia masazo katika nchi, na kuwaokoa ninyi kwa wokovu mkuu. Basi si ninyi mlionipeleka huku, ila Mungu; naye ameniweka kama baba kwa Farao, na bwana katika nyumba yake yote, na mtawala katika nchi yote ya Misri.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/