Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano
Neno lake lilikuwa na uwezo (m.32). Uwezo huo ulionekana kwa vile alivyowafundisha kwa maneno mazuri sana. Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu? ... Wakashangaa mno kwa mafundisho yake, kwa kuwa neno lake lilikuwa na uwezo (m.22, 32). Pia ulionekana kwa vile pepo mchafu alivyohangaika humo ndani. Kwake neno la Yesu lilikuwa kama moto, alijisikia kuangamizwa akisema, Acha! Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? (m.34). Pepo alikuwa na nguvu ya kuweza hata kumwangusha yule mtu. Ila kumdhuru hakuweza. Ndipo Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, mtoke. Ndipo yule pepo akamwangusha katikati, akamtoka asimdhuru neno (m.35). Tanzania nimeona mara kwa mara tukio kama hili. Nimeona kwamba hata leo Yesu ni mwenye mamlaka juu ya Shetani kama tulivyoona katika somo la juzi. Usihofu, maana Yesu anakupenda sana!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
http://www.somabiblia.or.tz